IDARA ya Uhamiaji Mkoani Mwanza imeendelea kuwanasa Wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa njia za panya baada ya hivi karibuni kuwakamata vijana watatu raia wa Burundi.
Akizungumza
ofisini kwake leo Naibu Kamishina Msaidizi na Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mwanza Bi. Anamaria Yondani alisema kwamba hii inatokana na Idara hiyo kuendelea
kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na kuzifanyia kazi, huku pia uhamiaji
ikiendelea kutekeleza mradi wa Shirika la Kimataifa ambalo linahusika na
shughuli za Kiuhamiaji (OIM) kupitia mradi wa Capacity Buiding in Migration
Management (CBMM-II)
Bi
Yondani aliwataja vijana hao waliokamatwa kuwa ni Akizmana Adamu (15), Gerlad
Michael (17) na Boaz Ernest (15) wote wakazi wa Ruingi raia wa nchi yaBurundi
walioingia nchini kwa njia za Panya kupitia Mkoani Kigoma kabla ya kunaswa
Mkoani Mwanza wakiwa kwenye harakati za kutafuta kazi ili kuwasaidia kuishi
nchini kinyume cha taratibu na sheria za nchi.
Kaimu
Mkuu huyo wa Uhamiaji Mkoa alisema tatizo la wahamiaji haramu limekuwa ni Janga
la Kitaifa na Mkoa wa Mwanza ni Kitovu cha Mawasiliano, Biashara ,Elimu na
Usafiri kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nchi za Maziwa Makuu na wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akitoa
taarifa ya Mkutano wa Kamati ya National Immigration Inter-regional Steering
Committee (NIISC) uliofanyika Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa Machi 11 hadi 12
mwaka kwa lengo la kuendeleza mradi wa CBMM-II, kuongeza Mikoa wanachama wa
NIISC na Namna ya kushirikiana na IOM katika kuendeleza mradi wa huo ambayo
yalijadiliwa katika mkutano huo.
“Mradi
huu wa NIISC awali ulianzisha na Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Kigoma mwaka
2012 na kasha kuongeza Mkoa wa Rukwaa hii ikumbukwe ipo katika Kanda ya Ziwa
ambapo kuna vivutio kadhaa vinavyosababisha wahamiaji haramu kuingia na
kujipenyeza katika sekta za i Uvuvi, Kilimo, Ufugaji, Madini, Biashara, Elimu na
Usafiri hali ambayo Uhamiaji imekuwa ikizifanyia doriawavutia ”alisema
Aidha
katika mkutano huo uliweza kuongeza wanachama wapya katika Kamati ya NIISC
ambayo ni Mikoa ya Geita, Shinyanga ,Tabora na Katavi ili kuongeza ushirikiano
katika kubadilishana taarifa na uzoefu wa utekelezaji wa majukumu ndaji ya kila
siku katika kupambana na wimbi kubwa la wahamiaji
haramu.
“Tunatambua
wahamiaji haramu bado wanaendelea kupitia nchini mwetu kwa ajili ya kuelekea
nchini Afrika ya Kusini ambapo awali walikuwa wakipita Mpaka wa Sirali kutokea
nchi ya Kenya kuingia Wilaya ya Tarime,Musoma kisha Mkoani Mwanza na kuelekea
Mikoa ya Kati hadi Mkoani Mbeya kabula ya kuanza safari kuelekea nchi za kusini
hadi Afrika Kusini ili kuwa lahisishia kwenda nchi za
Ulaya”alisema.
Bi
Yondani alisema kwamba baada ya kutekelezwa kwa mradi wa CBMM-II wahamiaji
haramu waliamua kubadili njia pengine kupita mawakala ambao ni raia wa Tanzani
wanaowasaidia kuwaingiza kwa njia haramu na sasa kupitia Mikoa ya Kaskazini ya
Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga na kuelekea mikoa ya Kati kwa ajili nya
kuelekea Mkoani Mbeya na kuvuka kuelekea Malawi na
Zambia.
“Lengo
kuu la wahamiaji haramu ni kwenda Afrika Kusini ni kutafuta maisha bora na kuwa
njia lahisi ya kwenda Mataifa ya Bara la Ulaya na Marekani huku wahamiaji wengi
wanaoingia kinyume na utaratibu wa kisheria wengi ni kutoka nchi za
Ethiopia,Eritrea na Somaliaambao wamekuwa wakinyanyaswa, kuteswa na kufariki
wanapokuwa safarini kwenye maroli ya mizigo na watu
wanaowasaidia”alisema
“Wanatumia
njia za panya kusafiri kupita mipaka isiyo rasimi na husaidiwa na mawakala
(Maajenti) wao ambao wengine ni watanzania wasio na uzalendo na wamekuwa
wakiwapakiza katika maroli ya mizigo,magari ya makontena na hata wengine
kupitishwa kwenye Hifadhi za wanyama wakali na baadhi yao kupitia Ziwa Victoria
kwa mitumbwi na kuvuka mito yenye wanyama wakali wakati wa
usiku”alieleza
Bi.Yondani
ametoa wito kwa wananchi kurejesha uzalendo wa Taifa na kushirikiana na maafisa
uhamiaji na polisi kutoa taarifa kwa watu ambao wanawahisi kuwa siyo raia na
watu ambao wameingia kwa njia za panya katika maeneo mbalimbali ya Mikoa yao na
wanaotafuta kujipenyeza kufanya kazi ambazo zitawasaidia kuonekana kuwa ni raia
wakati huu taifa linaelekea kutoa vitambulisho vya uraia
.
“Wananchi
sasa warudishe uzalendo wao na kuacha kuwasaidia wageni na wahamiaji haramu
walioingia nchini kinyume cha taratibu na kuvunja sheria za nchi kwa kuwatolea
taarifa kwa ofisi za uhamiaji na vituo vya jeshi la polisi kwa lengo la
kupambana na janga hili la kitaifa la kupambanana wahamiaji haramu wanaoingia
nchini kila siku kwa kusaidiwa na mawakala na kuhifadhiwa na watu wasiokuwa na
uzalendo”alisisitiza
Amevipongeza
vyombo vya habari kwa kushirikiana na Idara hiyo kutoa taarifa kwa wananchi
ikiwemo Elimu kwa kueleza bayana athari za kuwa na wahamiaji haramu ambao wengi
wao wamekuwa wakifanya uhalifu na kuwapora mali na kufanya mauaji kwa wananchi
na sasa wananchi katika maeneo yao ya mitaa na kata kuwa kuwatolea watu ambao si
raia ili kuwabaini kabla ya kutolewa vitambulisho vya uraia
kitaifa.
Credits: Gsengo
Credits: Gsengo
Post a Comment