Mwanafunzi wa kiume wa
mwaka wa pili sheria mwenye umri kati ya 22 mpaka 25 amejinyonga march 25 2013
pembeni ya madarasa chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo saa nne asubuhi mwili
wake ndio ulikutwa ukiwa unaning’inia kwenye mti, kwenye barua aliyoacha
ameandika asilaumiwe mtu.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Joseph Bernadina (25),
amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la
Yombo chuoni hapo.
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita
alipokea simu kutoka kituo cha polisi cchuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi
alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka
kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa
Jumapili.
“Nilikuja
tena kushituka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa
kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku akiwa na
karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe uliosema, kifo
chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa ridhaa yake --asisumbuliwe
mtu yeyote kwani nimefanya hivi kwa maamuzi yangu mwenyewe pia nizikwe
kwetu--” alisema.


Post a Comment