TENGA AHIMIZA VIGEZO U15
FIFA COPA COCA-COLA
Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika
michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola 2013.
Ametoa mwito huo leo
(Machi 26 mwaka huu) wakati akifungua semina elekezi ya michuano ya Copa
Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini
ya miaka 15.
Rais Tenga amesema hakuna
jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa
vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto
wapende kucheza mpira wa miguu.
“Kwanza nawashukuru kwa
kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha
mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika
semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya
yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga.
Pia ameishukuru kampuni ya
Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano hiyo tangu mwaka 2007 ambapo semina
hiyo elekezi inayoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na
waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ni ya saba
mfululizo.
Ratiba ya michuano hiyo
kuanzia mwaka huu imebadilika ambapo sasa itaanzia ngazi ya wilaya Aprili wakati
fainali katika ngazi ya Taifa itachezwa Septemba.
SIMBA, KAGERA SUGAR
KUPAMBANA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea kesho (Machi 27 mwaka huu) kwa mechi
mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa mgeni ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja huo wenye uwezo wa
kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenyen ushindi kutokana
na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.
Mechi nyingine itapigwa
kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kati ya wenyeji Azam
na Tanzania Prisons kutoka
Mbeya.
Post a Comment