Mkurugenzi Mtendaji wa
benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina, akizungumza na waanbdishi wa habari
Makoa Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam juu ya mchakato wa Matembezio ya
Hisani ya Step Ahead mwaka huu ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na yatakuwa ya
Kilometa 5 ambapo Mgeni Rasmni anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro. Pamoja nae
ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon.
Mkurugenzi wa AMREF
Tanzania Dr, Festus Ilako (kulia) akizungumzia ushiriki wa Shirika hilo katika
kufanikisha matembezi hayo ya Hisani ya Step Ahead mwaka huu
ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na yatakuwa ya Kilometa 5 ambapo Mgeni Rasmni
anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro. Pamoja nae ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Hospitali ya CCBRT, Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya
Barclays Tanzania, Kihara Maina.
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano cha Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akifdafanua jambo kwa
wanahabari juu ya matembezi hayo ya Hisani. Wengine katika picha ni Naibu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.
Waandishi wa Habari kutoka
vyombo mbalimbali vya Habari nchini Tanzania na Afrika Mashariki wakisikiliza
kwa makaini uzinduzi wa matembezi hayo ya hisani ambapo nawao wamehimizwa
kushiriki ili kuchangia Matibabu na afya ya mama na mtoto nchini.
****
****
Kila mwaka Benki ya
Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step
Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na Tanzania
walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo fedha
zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo
cha kansa cha Ocean Road.
Matembezi haya ya hisani
yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu wa benki
ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji
muhimu katika jamii. Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu
mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya
uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii
yetu.
Akiongea katika vyombo vya
habari leo, Ndugu, Kihara Maina, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays
Tanzania amesema, tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013 katika hoteli
ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita tano (5) na kila
mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa kwa shilingi za
kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya Barclays kuanzia
tarehe 29 Aprili, 2013
Susan Boon, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT
amesema “msaada huu ambao CCBRT wanaupokea kutoka Benki ya
Barclays ni wa thamani sana ambapo tunafanya kazi ili kufikia
malengo ya Tanzania ambapo jamii itajiwezesha kupaha huduma bora na salama hasa
kwa walemavu wa viungo na pia itawafikia wakinamama wote na kuhakikishia usalama
wao kwenye huduma ya afya ya uzazi na watoto
wachanga inafanikiwa. Mkakati huu wa benki ya Barclays Step Ahead utasaidia pia
katika kukinga mapungufu ya mtindio wa ubongo na fistula hapa Tanzania, na vile
vile kuhakikisha kwamba wale waliopata mapungufu wakati wa kuzaliwa wanapata
matibabu katika sehemu za viungo vyao haraka iwezekanavyo.
Pia kwa kushirikiana na
taasisi zetu za hapa nchini CCBRT na benki ya Barclays Tanzania tunakusudia kuwa
mfano mzuri na muhimu katika jamii inayotuzunguka na tunafutrahia sana kuwa
chachu ya msaada katika jamii yetu inayotuzunguka ya Tanzania.”
Akiongea pia na waandishi
wa habari katika mkutano na vyombo vya habari, Dr, Festus Ilako Mkurugenzi wa
AMREF Tanzania amesema “Msaada na mkakati huu wa benki ya Barclays Tanzania kwa
AMREF ni wa kila wakati, na kwa pamoja tunaweza tukaibadilisha jamii kutoka
ilipo katika masuala ya afya kwa wakina mama na watoto, hivyo kuitengenezea
jamii uelewa na ustadi katika kusimamia afya njema na kuvunja marudio
rudio ya ufukara katika afya na umaskini.
Kampeni hii kutoka benki ya
Barclays ijulikanayo kama Step Ahead itasaidia kuelimisha wakunga na wazalishaji
katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na kuwawezesha wakina mama wajawazito
kujifungua katika mikono ya salama ya wafanyakazi waliofuzu katika Nyanja ya
afya hivyo kupunguza uchangiaji wa vifo visivyo lazima na ulemavu wa viungo kwa
mama na watoto chini ya miaka mitano. Ushirika huu baina ya
Barclays na AMREF ni mfumo mpya ambayo utawezesha jamii kupata
ubora na unafuu katika masuala ya kiafya.
Mwaka 2011, Benki ya
Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za kitanzania
milioni 150 kutokana na mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka
kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi
milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine
katika jamii.
Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa
uzazi
2. Matibabu ya Fistula
3.Upasuaji kwa watoto
waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi
Step Ahead Walk 2013
itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya
kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili tuweze kufanya
badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania hususani masuala ya
uzazi na afya ya watoto.
credits: Father Kidevu
Post a Comment