Juma Pinto Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA akitangaza bendi ya muziki itakayotumbuiza
kwenye bonanza la waandishi wa habari litakalofanyika Aprili 6 Jumamosi
kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu
wa TASWA Amiri Mhando na kulia ni Doris Malulu Ofisa Uhusiano TBLWanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo wakiwa katika mkutano huo.Ali
Choki Mzee wa Farasi kutoka bendi ya Extra Bongo akizungumza na
waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika kwenye mgahawa wa City
Sports Lounge kulia ni Super Nyamwela mnenguaji wa bendi hiyo kutoka
kushoto, Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando , Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na Doris Malulu Ofisa Uhusiano TBL.
……………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya Extra
Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern ndiyo burudani
zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es
Salaam kesho (Jumamosi).
Akizungumza
Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti wa
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinachoandaa
bonanza hilo, Juma Pinto alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo
linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.
Alisema
wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern
inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa
katika muziki kwa maeneo yao.
“Tunaamini
watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na
tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo
litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi
atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Pia
Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo
kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza
kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka
kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.
“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
Bonanza
hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na
lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa
siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa
vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi
pamoja.
Kwa
upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema wamejipanga vya
kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda
kama yalivyopangwa.
“TBL
ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba
msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka
vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo
watafurahi vya kutosha siku hiyo.
Naye
Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga
vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari
wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi
kuiona Extra Bongo.
Post a Comment