Warembo watakaowania taji la
Redd's Miss Dar Indian Ocean wakimsikiliza kwa Umakini Mkurygenzi Mkuu
wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss
Tanzania,Hashim Lundenga wakati alipowatembelea warembo hao kwenye kambi
yao ya Mazoezi.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert
Makoye.
*********
HATUA za awali za kumsaka Redd’s
Miss Tanzania sasa zinaanza kushika kasi, wakati wiki hii kutakapokuwa
na kinyang’anyiro katika vitongoji kadhaa vya kusaka warembo wao.
Kazi kubwa itaanza Morogoro,
wakati atakaposakwa Redd’s Miss High Learning atakayeuwakilisha mkoa huo
katika kumpata mrembo kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu, shindano
litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sirvoy
Wakati Morogoro Miss High Learning
akipatikana kesho, shughuli pevu ipo keshokutwa (Jumamosi) pale
kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s Miss UDOM, litakalofanyika
katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma
Siku hiyo pia atapatikana
mwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Kagera na Mwanza, shindano
ambalo litafanyika Yacht Club, Mwanza.
Akizungumzia kuhusu Redd’s Miss
Morogoro High Learning, mratibu wa shindano hilo, Verdian Kamugisha
alisema kila kitu kimekamilika na kutakuwa na burudani za kufa mtu.
“Tumekamilisha kila kitu na
warembo wote wako katika hali nzuri na kutakuwa na burudani za kumwaga,
wakazi wa Morogo wanatakiwa kuja kwa wingi kushuhudia kile
kitakachotukia,” alisema.
Mratibu wa Shindano la Redd’s Miss
UDOM, Rachel Matina naye alisema kila kitu kwao kipo tayari na watu
wanatakiwa kufika kwa wingi kushuhudia jinsi warembo kutoka Chuo Kikuu
Dodoma, walivyopania kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwaka huu.
Joseph Rwebangira wa anayeratibu
shindano la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mikoa ya Kagera na
Mwanza naye alikiri kukamilika kwa maandalizi yote na kutakuwa na
burudani za kila aina siku ya onyesho.
Upande wa kanda ya kaskazini mwa
nchi kutakuwa na shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Hai ambapo
shindano hilo linatarajiwa kufanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Snow
View na mkoani Mara katika kitongoji cha Tarime shindano litakuwa katika
ukumbi wa JJ Club na maandalizi kwa sehemu zote husika yameshakamilika
kwa kiwango kikubwa.
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
LUKAZABLOG
Post a Comment