KILIMO
KUTUMIA SHS. 328,134,60 8,000 KATIKA MWAKA WA FEDHA
UJAO
SERIKALI
ITAENDELEA KUWAENDELE
SERIKALI
IMEFANIKIW
Habariz zote
za Bunge na Benedict Liwenga-Maelezo,
Dodoma.
|
Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika inatarajia kutumia jumla ya shilingi
328,134,608,000/- katika mwaka ujao wa fedha.
Takwimu
hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.
Alisema
kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 247,094,320,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya
kawaida na Shilingi 81,040,288,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya
maendeleo.
Chiza
aliongeza kuwa Shilingi 210,175,943,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC)
kwa ajili ya Wizara hiyo .
Aidha
,shilingi 25,602,969,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Wizara na
Shilingi11,315,408,000 ni Mishahara (PE) ya Bodi na Taasisi zote zilizoko chini
ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kwa upande
shughuli za maendeleo, Chiza alisema kuwa Wizara hiyo imetenga kiasi cha
shilingi 23,927,000,000 ikiwa ni fedha za ndani na shilingi 57,113, 288,000 ni
fedha za Nje.
Wabunge
wanatarajia kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika kwa
kipindi cha siku mbili ambapo itahitimishwa kesho.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe. Chiza amesema Serikali
inatarajia kufufua Kituo cha Kilimo Anga ili kukiwezesha kuwa na ndege na
Wataalam watakaosaidia kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa
Nzige.
Mhe. Chiza
amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege kukodi
kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa
jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati
zinazohitajika.
Kufuatia
hali hiyo amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya
kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa
ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
*******
*******
SERIKALI
ITAENDELEA KUWAENDELE ZA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO
NCHINI
SERIKALI inatekeleza
mkakati wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini kwa kuwatambua
wao na mahitaji ya mitaji na vifaa ili kutekeleza kazi yao kwa
ufanisi.
Kauli hiyo imetolew na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Julius Masele wakati akijibu swali na
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani leo mjini Dadoma aliyetaka
kujua ni lini wachimbaji wadogo wadogo wa Ng’ombeni, Kalalami, Kigwase
watatambuliwa na Serikali na kupewa kipaumbele kwenye uchimbaji, na kupewa
mikopo ya kujikimu wakati wakitafuta Madini.
Amesema kuwa katika
kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo wadogo Wizara hiyo imeshakwishatoa imetoa
jumla ya viwanja 612 vya uchimbaji mdogo wa madini katika maeneo ya Ng’ombeni,
Kalalani na Kigwase ikiwa ni hekta 3,864.
Aidha, Naibu Waziri huyo
ameongeza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa na Wakala wa Jiolojia
inaendelea kubainisha maeneo yanayofaa kwa uchimbaji mdogo ili yaweze kutengwa
kisheria na kugawiwa kwa wachimbaji hao.
Masele alisema kuwa
katika utekelezaji wa mkakati huo unashirikisha wachimbaji wenyewe kwa
kuimarisha vyama vyao vya kimkoa na chama cha kitaifa (FEMATA) na kujadili
masuala yao katika vikao vya pamoja vya kila baada ya miezi sita baina ya
wawakilishi wao na Wizara.
Ameongeza kuwa Wizara ya
Nishati na Madini inakamilisha taratibu za Mfuko rasmi wa kuwaendeleza
wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata mikopo ya vifaa vya uchimbaji wenye
tija.
Aidha , Naibu Waziri
huyo amewasisitiza wachimbaji wadogo wadogo kuwa mikopo hiyo wanayopata inapaswa
itumike vizuri katika malengo waliyoombea ili wajihakikishie kuzalisha madini
mengi na kujiongezea kipato.
*******
********
UDHIBITI WA VISUMBUFU VYA MAZAO
SERIKALI
itafufua kituo cha Kilimo Anga kwa kukiwezesha kuwa na ndege na Wataalam ili
kujenga uwezo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko kudhibiti milipuko ya
visumbufu vya mazao hasa Nzige.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza
wakati akiwasilisha Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo
leo.
Mhe.
Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege
kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa
jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati zinazohitajika hali ambayo
husababisha Wizara kutegemea kukodisha ndege kutoka sehemu
nyingine.
Amesema
Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi
(Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa ndege
moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
Aidha,
Wizara itaweka utaratibu wa kuingia ubia na makampuni binafsi na taasisi
zinazotoa huduma kama hizo ili kukijengea uwezo kituo cha Kilimo
Anga.
Wakati
huo huo, Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula ilisambaza lita ,6000 za
kiuatilifu cha kudhibiti milipuko ya viwavijeshi katika mikoa ya Rukwa, Katavi,
Mbeya, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita. Dodoma, Morogoro na Tanga kunusuru
hekta 16,418 za mazao ya nafaka.
******
*******
SERIKALI
IMEFANIKIW A KUONGEZA WATAALAM WA KILIMO NCHINI HADI KUFIKIA
7,974
Wataalam wa ugani
wameongezeka kutoka 3,379 waliokuwepo mwaka 2007 hadi kufikia 7,974 mwezi Juni
jana(2012) baada ya Serikali kuajiri wahitimu kutoka vyuo mbalimbali
nchini.
Hayo yamesemwa leo mjini
Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Adam Kighoma Malima
wakati akijibu swali Mhe. Mch. Dk. Getrude Rwakatare (Viti Maalum kupitia Chama
cha Mapinduzi).
Amesema kuwa mwaka 2007
Serikali ilifanya tathmini ya upatikanaji wa huduma za ugani nchini na kubaini
kwamba mojawapo ya vikwazo vikubwa vya upatikanaji wa huduma za ugani kwa
ufanisi nchini ni upungufu mkubwa wa wataalam.
Malima ameongeza kuwa
matokeo ya tathmini hiyo yalionyesha kuwa kulikuwepo na wataalam 3,379 nchini
ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wataalam 15,082.
Amesema katika
kukabiliana na changamoto hiyo , Serikali ilianza kutekeleza Mpango wa
kuimarisha huduma za Ugani nchini ambapo kuanzia mwaka 2007 Serikali imevifufua
vyuo 13 vya kilimo nchini (MATIs) vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na
Ushirika.
“Ukarabati mkubwa wa
vyuo vitatu MATI Ukiriguru, Maruku na Naliendele-Mtwara na ukarabati mdogo kwa
baadhi ya vyuo kumi vingine umefanyika”. Mhe. Malima
alisema.
Aidha, Mhe. Malima
amesema kuwa vyuo viwili vya mashirika yasiyo ya kiserikali vilishirikishwa
katika kutoa mafunzo yaliyolenga kuongeza idadi ya wataalam wa Ugani na vyuo
hivo kwa sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi 3,500 kwa wakati mmoja
ikilinganishwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 uliokuwepo kabla ya mwaka
2007.
Post a Comment