IMEELEZWA kwamba inakadriwa kuwa asilimia saba ya idadi ya watu wazima wanaugua ugonjwa wa kisukari, lakini chini ya 1/3 ndio wanaofahamu wana tatizo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (Pichani) wakati akizindua kliniki ya vikoba ya wagonjwa wa kisukari uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dares Salaam.
Dk. Mwinyi alisema watu wanaokabiliwa na tatizo hilo, wanafika hospitalini wakiwa wameathirika figo, macho, shinikizo la damu au kukatwa miguu.
“ Ninaishauri jamii kutumia huduma hiyo ili kuweza kuchunguza afya zao na kujinga kwa kufuata kanuni za afya kama vile kula vyakula visivyo na mafuta mengi, sukari nyingi, chumvi kiasi, kula mboga za majani kwa wingi na matunda,” alisisitiza. Dk. Mwinyi.
Aliongeza pia jamii inatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha, kupunguza uzito kwa kiwango kinachotakiwa, kutovuta sigara na kupunguza kunywa pombe au kuacha kabisa.
Dk.Mwinyi alisema 1/3 ya idadi ya watu wazima wanakabiliwa na shinikizo la damu, lakini chini ya asilimia 10 ndio wanafahamu kuwa wameathirika na tatizo hilo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania, Dk.Kaushik Ramaiya alisema kliniki hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano wa chama hicho na wizara hiyo ili kuboresha huduma za afya nchini.
Pia imetolewa na Novo Nordisk wakishikikiana na Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Duniani.
Alisema kliniki hiyo ambayo itakuwa na inatoa tiba kwa wagonjwa wa kisukari hususan watoto inafaa vifaa vya kisasa kwa ajili ya upimaji wa matatizo ya kisukari ,macho,meno na mahabara ikiwemo genereta itakatotumika sehemu ambazo hazina umeme . Pia itatoa huduma hiyo kwa watu wazima .
Aliongeza kuwa kliniki hiyo ni ya kwanza kuzinduliwa ni maalum kwa kanda ya ziwa ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi. Hivyo hapo baadae watatoa nyingine kwa ajili ya kanda zingine.
Katika uzinduzi huo jumla ya watu wapatao 79 walijitokeza kupima afya zao na kupata ushauri mbalimbali.
Post a Comment