Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,wama, Mama Salma Kikwete akipokewa
rasmi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Jhpiego nchini Tanzania, Bi
Maryjane Lacoste kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki kulikofanyika
sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika hilo tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipata maelezo kutoka kwa Dr. Maryrose Giattas, Cervical Cancer
Prevention Program Adviser wa Shirika la Jhpiego kwenye maonyesho ya
huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo. Maonesho hayo yalifanyika
katika hoteli ya Doubletree ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 40 ya
shirika hilo.
Mama Salma Kikwete akipata maelezo
kutoka kwa Dr. Hokororo wa shirika la JHPiego juu ya kuhifadhi vifaa
vinavyotumika katika suala zima la afya ya mama na mtoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka 40
ya shirika la Jhpiego huko Doubletree hotel Masaki. Kulia kwa Mama Salma
ni Dr. Leslie Mancuso, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego akifuatiwa na
Bi Sharon Cromer, Mkurugenzi wa Shirika la USAID nchini Tanzania. Kulia
ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid akifuatiwa na
Dr Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice President na wa mwisho ni Mkuu wa
wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye
sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego wakisikiliza hotuba
ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA
Mama Salma Kikwete akihutubia kwenye sherehe za kutimiza miaka 40 ya
shirika la JHPiego kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki jijini Dar es
Salaam tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwashirikiana na viongozi wengine kukata keki ya kutimiza miaka 40 ya
shirika la Jhpiego zilizofanyika katika hoteli ya Doubletree. Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID Bi. Sharon Cromer, Rais na Mtendaji
Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso, Mama Salma, Bi Maryjane Lacoste,
Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Tanzania, Dr. Seif Rashid, Naibu Waziri wa
Afye na Ustawi wa Jamii na Dr. Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice
President.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akigongainisha glass yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie
Mancuso ikiwa ni kusherehekea kutimiza miaka 40 kwa shirika hilo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipongezana na Rais wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso mara baada ya kukata
keti ya kutimiza mika 40 ya shirika hilo katika sherehe zilizofanyika
huko Doubletree hotel tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwaaga kwa kuwapungia mikono washiriki waliohudhuria sherehe za
kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego. PICHA NA JOHN LUKUWI
Post a Comment