KIUNGO wa Toto African ya Mwanza, Emmanuel
Swita amesema anajipanga kwenda Mahakamani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka,
kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' kumtishia
maisha.
Ugomvi wa wawili hao ulianza mara baada ya
kocha Jamhuri Kiwhelo kudokezwa na mashabiki uwanjani hapo kuwa mchezaji huyo
amechukua mpira uliodaiwa kuwa ni mali ya klabu ya Simba.
Julio baada ya kupata habari hizo alipanda
kwenye gari la Toto African na kuchukua ufunguo wa gari kushinikiza gari hilo
halitaondoka hadi mpira huo utakapopatika.
"Kweli nilikuwa na mipira ambayo ni mali ya
timu ya Toto kuiweka kwenye gari. Nadhani ni kitu ambacho kiliwafanya mashabiki
kuhisi ni mimi niliyechukua mpira wa Simba."
"Julio alivyopanda kwenye gari alichukua
ufunguo kwa dreva kuzuia gari isiondoke huku akitupiana maneno na
wachezaji."
"Kwa suala la kumpiga ngumi sijui aliyempiga.
Nimesikia akinishutumu kwenye vyombo vya habari kuwa mimi ndiye niliyempiga na
kunitishia maisha."
Swita alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa
ameongea na viongozi wa timu yake kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Julio
kumtishia amani na kumuunga mkono kwa uamuzi huo.
"Tarifa ambazo nimesikia akitangaza kwenye
radio ni kwamba hataondoka Mwanza mpaka atakapolipa
kisasi."
"Kwa hiyo, ili kujiweka katika hali ya
usalama na hilo naenda kukata 'RB' na viongozi wangu wameniahidi kunipa
ushirikiano wa kutosha." alisisitiza mchezaji
huyo.
Post a Comment