TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KAMATI Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa siku mbili kwenye kikao chake
cha kawaida jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 3-4 Machi,
2013.
Katika kikao hicho cha
siku mbili, Kamati Kuu itajadili pamoja na mambo mengine, yatokanayo na kikao
kilichopita, hali ya kisiasa nchini pia itapokea taarifa ya maendeleo ya
maazimio ya kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika mwezi Februari mwaka huu,
ikiwemo mpango wa uendeshaji chama kwa kanda.
Aidha, Kamati Kuu pia
itajadili mpango kazi na bajeti ya Chama kwa mwaka 2013-2014
Imetolewa, Dar es Salaam
na;
Tumaini
Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari
CHADEMA
Post a Comment