Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja.
Baada ya Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 ambayo
imeanza upya kwa kasi ya ajabu ambapo wadau mbali mbali ikiwa ni asasi za
Serikali, Taasisi mbalimbali, Makampuni pamoja na watu mbalimbali wamejitokeza
kudhamini Fainali Hizo za Miss Utalii Tanzania Taifa Ambazo zitafanyika
Mwanzoni mwa Mwezi Ujao.
Walio jitokeza
Kudhamini ni pamoja na. TANAPA, Ngorongoro Crater, Tanzania Tourist Board,
Mtwana Catering, Ikondolelo Lodge Hotel, Sahara Media Group, Mbasha Entertainment,
Sophia Records,Nyinda Hotel, Tanga Beach Resort, Retco, Tanzania School of
Journalism and Mass Communication,
Oriental Berau De Change, Clouds Media Group, Times FM, Global
Publishers, Tone Multimedia Group Dar es salaam City College, Eden Hill
College, Maweni Hotel.
Bado kuna wadau
wengine mbalimbali ambao wanaendelea kujitokeza kwa ajili ya Kudhamini Fainali
Hizo za Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Mpaka sasa Kambi mpya ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 ipo na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30
wamejiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika Mwanzoni
mwa mwezi Ujao ikiwa ni pamoja na Kutoka Mikoa yote Tanzania, Kanda Maalum ya
Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism University World, Miss Globe International n.k
Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality n.k
Post a Comment