Ispekta Generali wa Polisi
(IGP), Said Mwema.
Na Bryceson Mathias,
Mvomero
JESHI la Polisi wilayami
Mvomero, limefanikiwa kutuliza vurugu za uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa
mabaraza ya katiba ya wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) na uendeshaji wake
uliotangazwa na tume ya mabadiliko ya katiba.
Uchaguzi huo uliokuwa
ufanyike jana Kichamgani Turiani, ulkwama kufanyika, baada ya kuibuka vurugu
wananchi wakimkataa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Bw. Damson Minja
asiwe Mwenyekiti wa kikao kwa sababu ameshindwa kusoma mapato na matumizi tangu
achaguliwe.
Diwani wa Kata ya Mhonda Bw.
Salum Mzugi na viongozi mbalimbali wa CCM walishindwa kutuliza na kurejesha
Amani kwa sababu badala ya kutatua Vurugu hizo kwa kufuata Mwongozo, taratibu na
Sheria za Uchaguzi huo, walitanguliza Itikadi jambo lililosababisha Polisi
kuingilia Kati wakiwa tayari na Mabomu ya Machozi.
“Vurugu ilifikiwa pale
Viongozi wa CCM walipolazimisha Wananchi waongozwe na Mwenyekiti Minja
wasiyemtaka ambapo walishatangaza kumng’oa kwa kushindwa kusoma mapato na
matumizi tangu achaguliwe 2010. Hivyo Chadema kuona CCM inataka
kuwaburuza”.alisema Diwani wa Viti Maalum Bi. Juliana Petro
(CHADEMA).
Sinema iliyokuwepo kwenye
Kiti cha Mwenyekiti ilikuwa, Mwenyekiti Bw. Minja akitaka kukaa kwenye kiti,
Kiti hicho kilikuwa kimavutwa na Wananchi wanaopinga, Jambo lilizua ubishani wa
kisiasa baina CCM na CHADEMA, hadi kusababisha viongozi hao wa Mabaraza
kutochaguliwa.
Aidha Jeshi la Polisi Kituo
cha Turiani kupitia kwa Kamanda Rajab Shemndolwa liliagiza, viongozi husika
watafute mwongozo wa Taratibu na Sheria zinazotakiwa kufuatwa katika kutatua
mgogoro huo toka kwenye vyombo husika, ila hawataki vurugu, na zikitokea
hawatasita kuchukua hatua za maamuzi magumu.
Mgogoro wa wananchi wa
Kichangani Turiani kumkataa Mwenyekiti wao Bw. Minja, umedumu kwa miaka mitatu
sasa bila kutatuliwa na viongozi husika katika kata na wilaya ya mvomero, tatizo
likiwa ni Serikali ya mwenyekiti huyo kutosoma Mapato na Matumizi jambo ambalo
lisipotatuliwa, linaweza kuleta maafa baadaye.
Post a Comment