* Laomba hatua
zinazochukuliwa ziwe endelevu kukomesha majanga ya
kizembe.
NA
MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umelezea kusikitishwa kwake na matukio ya watu kupoteza maisha na kujeruhiwa yaliyotokea mapema wiki hii, likiwemo la kuporomoka jengo la ghorofa 16, jijini Dar es Salaam, na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhiwa wengine kadhaa.
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umelezea kusikitishwa kwake na matukio ya watu kupoteza maisha na kujeruhiwa yaliyotokea mapema wiki hii, likiwemo la kuporomoka jengo la ghorofa 16, jijini Dar es Salaam, na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhiwa wengine kadhaa.
Tukio lingine lingine ni
lililotokea juzi, Aprili mosi, ambako watu zaidi ya watu 20 wameelezwa kupoteza
maisha baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu, eneo la
Chekereni mkoani Arusha.
Katika taarifa iliyotolewa
na Makao Makuu ya UWT jijini Dar es Salaam, leo, Aprili 3, 2013, Katibu Mkuu wa
Jumuia hiyo, Amina Makilagi amesema, UWT pia inalaani matukio ya kuchinjwa kwa
wanawake yanayoendelea kutokea Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara ambapo taarifa
zilizopo Mwanamke mmoja amechinjwa kinyama kwa kutenganishwa kichwa na
kiwiliwili chake na watu wasiojulikana.
” UWT imesikitishwa na
vitendo vya kinyama vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio na moyo wa kibinadamu
kwa kuwakata vichwa wanawake na kuondoka navyo kwa malengo yao binafsi hivyo
kusababisha wanawake kuishi katika maisha ya wasiwasi katika nchi yao”, alisema
Amina katika taarifa hiyo.
Alisema, UWT inaungana na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maelekezo mazito kwa mamlaka husika
kuchukua hatua kali kwa wahusika wa matukio yote.
Hata hivyo UWT imeomba
hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya majanga hayo, ikiwemo kuporomoka kwa
ghorofa, watu kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo na watu kukatwa vichwa, ziwe
hatua endelevu kuhakikisha matukio hayo hayatokei tena
kirahisi.
“UWT pamoja na kutambua
hatua za awali zilizochukuliwa hadi sasa katika matukio hayo, inaiomba Serikali
kuhakikisha hatua inazochukua sasa ziwe ni endelevu ili kuhakikisha matukio kama
haya ambayo kwa sehemu kubwa yanatokana na uzembe hayatokei tena”, alisema
Makilagi katika taarifa hiyo na kuongeza;-
“UWT inaungana na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Rais Kikwete kwa kutoa maelekezo mazito kwa mamlaka husika kuchukua
hatua kali kwa wahusika wa matukio yote”.
Amina aliwaombea ndugu
jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
maombolezo ya wapendwa wao ambao wameacha pengo katika familia zao na Taifa kwa
ujumla na kuwaombea wapone haraka
waliojeruhiwa
Post a Comment