Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa
(kushoto) na Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn
wakimshuhudia mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph,wakati akionesha kwa vitendo jinsi
chaja mpya aina ya Readyset inavyounganishwa kabla ya matumizi,uzinduzi wa chaja
hiyo inayotumia nishati ya jua,ina uwezo wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku,
matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye
kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi
ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na
Kampuni ya Fenix International.
Mkazi wa Pangani, Wilaya ya Kibaha, Pwani, Anna Joseph,
akionesha waandishi wa habari jinsi ya kutumia aina mpya ya chaja inayotumia
nishati ya jua 'ReadySet' iliyozinduliwa Dar es Salaam kwa ushirikiano wa
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom na Fenix International. Mkazi huyo amewaeleza
waandishi wa habari kuwa amekuwa akijipatia kipato cha hadi sh elfu 80 kwa mwezi
kupitia kifaa hicho kwa kuchajisha simu za wateja wake.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa
(kushoto)na mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph ambaye ni mmoja wa wadau walionufaika
na huduma ya chaja za Readyset,wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
namna chaja hizo mpya na zinatumia nishati ya jua zinavyofanya kazi .
Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo
yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya
Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix International. Wanaoshuhudia nyuma ni
Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn, na
Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International,nchini, Peter Mungoma.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin
Twissa, akisisitizia umuhimu wa kila mtanzania hususan wajasiriamali waishio
maeneo yasiyo na umeme kutumia aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya jua
maarufu Readyset ambayo pamoja na mambo mengine ina uwezo wa kuchaji simu zaidi
ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi
na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo
nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Kampuni ya
simu za mikononi ya Vodacom na Kampuni ya Fenix International
Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International, Peter
Mungoma akionyesha kupitia 'projector' aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya
jua, maarufu kama 'ReadySet Charger' ambayo pamoja na mambo mengine ina uwezo
wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa
hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho
hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia
ubia baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom na Kampuni ya Fenix
International
---
Dar es Salaam, Aprili 5, 2013 -
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imezindua chaja mpya
za simu 'Readysety' zinazotumia nishati ya jua na zenye uwezo wa kuchaji zaidi
ya simu 5 tofauti kwa wakati mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha watanzania
hususan waishio maeneo yasiyo na umeme kupata mawasiliano ya uhakika kupitia
simu zao za mikononi.
Readysety hizo pamoja na mambo mengine zinatumika kuzalisha mwanga kwa balbu ya aina yoyote kwa matumizi ya nyumbani na mahala pa biashara, na zaidi zina viunganishi kwa matumizi ya umeme wa kawaida.
Kukamilika na hatimaye uzinduzi wa chaja ya ReadySety ni matokeo ya ushirikiano wa kibiashara baina ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini na Fenix International baada ya kujiridhisha juu ya ubora na faida zake kwa watanzania hususan wajasiriamali waishio maeneo yaliyo nje ya gridi ya taifa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, kwenye duka la Vodacom, MlimaniCity, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom nchini, Rene Meza, alisema ReadSety zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza fursa za mawasiliano na uhitaji zaidi wa simu za mikononi kwa watanzania waishio maeneo yote mjini na vijijini
"Watanzania waishio nje ya gridi ya taifa, ambao mara kadhaa hupata adha ya kusafiri umbali mrefu pale wanapohitaji fursa za nishati ya umeme kwenye kuchaji simu zao sasa wamepata jawabu," alisema Meza na kuongeza:
"Zaidi ya watu bilioni 1.3 duniani wanaishi bila huduma ya umeme na kuna watumiaji wa simu za mikononi takribani milioni 600 wanaoishi bila kutumia umeme wa gridi kitu ambacho kinawalazimu kutumia karibu dola za Kimarekani bilioni 10 kila mwaka kwa ajili ya kuchaji simu kwa kutumia jenereta na betri za magari," alisema Meza
Aliongeza kuwa Kampuni ya Vodafone na Vodacom ina watumiaji wa simu zaidi ya milioni 100 duniani kote ambao hawajaunganishwa na gridi ya umeme ambapo kati ya hao Tanzania ni asilimia 14 ya idadi yote ya watu wapatao milioni 46 walio ndani ya gridi ya nishati ya umeme.
Aidha Meza, alisema kuwa majaribio yaliofanyika mwaka jana katika mkoa wa Pwani, yameonesha kuwa chaja hizo za ReadySet zimeweza kutoa fursa ya biashara kwa wajasiriamali, wakiwemo mawakala wapatao 40,000 wa huduma ya M-Pesa nchini.
Uzinduzi wa ubia huo wa kibiashara, unatarajia kuongeza kasi ya mahitaji ya simu za viganjani kwa watanzania sanjari na kuimarisha zaidi huduma ya M-Pesa ambayo hadi sasa imekuwa mkombozi kwa wateja zaidi ya milioni 4.5 nchi nzima.
"Kimsingi katika hatua ya majaribio iliyokwisha fanyika kwa baadhi ya mikoa nchini imeonesha ReadSety imesaidia kuongeza asilimia 14 ya usajili wa kadi za simu na mauzo ya muda wa maongezi kwa wastani wa pato la mtumiaji," alisema
Naye Meneja wa Biashara wa Fenix International, Peter Glenn alisema: "Kampuni ya Fenix International inaona fahari kuungana na Vodacom katika uzinduzi wa huduma ya chaja ya ReadySet Power System."
"Chaja hii ya kipekee ya ReadySet ni fursa nzuri kibiashara, na pia ni teknolojia rahisi kwa matumizi, ambayo bila shaka itasaidia kuboresha maisha kwa wateja wa simu za mikononi na wafanyabiashara ndogo ndogo walio nje ya umeme wa gridi ya taifa katika kujiongezea kipato," alisema Glenn na kuongeza:
"Gharama za ReadySety moja ni dola 200 sawa na Tsh 320 ambapo ikitumika vizuri itazalisha kati ya sh 64 hadi 80 kwa mwezi," alisema.
Mwisho ...
Post a Comment