Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani
Athumani
MBEYA, DAR ES SALAAM.
WATU 45
watafikishwa mahakamani wakihusishwa na vurugu zilizozuka juzi katika Mji wa
Tunduma.
Vurugu kubwa ziliibuka juzi kwenye Mji mdogo wa
Tunduma ambao ndiyo Makao Makuu ya Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya kwa baadhi ya
wakazi kuwa na mvutano mkali kuhusu nani anayepaswa kuchinja mifugo baina ya
waumini wa Kikristo na Waislamu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani
alisema jana watu 94 ndiyo waliokamatwa kutokana na vurugu
hizo.
Diwani alisema watu 49 wameachiwa kwa dhamana huku
uchunguzi ukiendelea wakati waliobakia 45 ndiyo watafikishwa
mahakamani.
Vurugu hizo
za Tunduma zilihusisha uchomaji wa matairi barabarani, kuweka mawe na magogo kwa
lengo la kufunga barabara na kusababisha shughuli za kiuchumi kusimama na
wananchi kujifungia ndani kwenye nyumba
zao.
Diwani alidokeza, hata hivyo, hali ya utulivu imerejea
kama kawaida na kwamba tayari wananchi wanaendelea na shughuli zao za kawaida
ikiwa ni pamoja na eneo la
mpakani.
Post a Comment