--
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza,
imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela Meneja wa Benki ya CRDB wa
matawi ya Nyanza na Bugando mkoani Mwanza, Daniel Peter Waijaha, pamoja
na mteja wa benki hiyo, Dismas Mohamed Ndaliko baada ya kuwakuta na
hatia wa kosa la wizi wa jumla ya Sh Milioni 140 mali ya benki hiyo.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza,
Anjelo Rumisha ambaye alikuwa akisikiliza kesi hiyo ya jinai Na.76 ya
mwaka 2011.Ambapo mbali na adhabu hiyo pia hakimu huyo amemtaka meneja
huyo azirejeshe fedha hizo alizoziiba katika Tawi la Nyanza.
Hakimu
Rumisha alisema baada ya kumtia hatiani meneja huyo pia Meneja wa
Business Banking, Stephano Harry Mboma, ambaye alikuwa mshatakiwa wa
pili katika kesi hiyo amemuachia huru baada ya kuona hana hatia katika
mashitaka dhidi yake.
mashitaka dhidi yake.
Kwa
upande wake Ndaliko (mteja) ambaye alikuwa mshtakiwa wa tatu katika kesi
hiyo alihukumiwa adhabu hiyo kwa kosa la kujaribu kumsaidia meneja huyo
kuepukana na adhabu kwa kufuta ushahidi wa kosa hilo.
Wakati
meneja huyo na mteja wakihukumiwa adhabu hiyo, Meneja wa Business
Banking, Stephano Harry Mboma, ambaye alikuwa mshatakiwa wa pili katika
kesi hiyo ameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hana hatia katika
mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza,
Jumatatu ya Juma hili, Anjelo Rumisha, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.
Hata
hivyo licha ya kuwatia hatiani washtakiwa hao kwa mashtaka hayo, na
kuwahukumu adhabu hiyo, Hakimu Rumisha aliwaachia huru katika mashtaka
mengine yote yaliyokuwa yakiwakabili.
Upande wa
mashtaka uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, David
Kakwaya haukuridhika na uamuzi huo wa washtakiwa hao kuachiwa huru
katika mashtaka mengine, na tayari umewasilisha taarifa ya kusudio la
kukata rufaa.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote kwa pamoja walikuwa
wakikabiliwa na jumla ya mashtaka matano, lakini ni mashtaka mawili tu
ndio yalikuwa yakiwahusu washtakiwa wote watatu, ambayo ni kula njama
kutenda kosa na kughushi.
Katika
shtaka la kwanza washtakiwa wote walikuwa wakidaiwa kuwa katika tarehe
tofautitofauti katika miezi isiyofahamika, mwaka 2010, walikula njama
kutenda kosa la kughushi nyaraka.
Shtaka la
pili lilikuwa ni la wizi likiwahusu mshtakiwa wa kwanza Meneja Waijaha
na mshtakiwa wa pili, Mboma. Walidaiwa kuwa katika tarehe na miezi
isiyofahamika mwaka 2010, kwa pamoja waliiba Sh 107.8 milioni katika
benki hiyo tawi la Nyanza.
Shtaka la
tatu ambalo pia ni wizi lilikuwa likiwahusu mshtakiwa wa kwanza,
Waijaha na wa tatu, Ndaliko (mteja). Walidaiwa kuwa Desemba 4, 2010,
katika benki hiyo tawi la Bugando, waliiba Sh32.15 milioni mali ya benki
hiyo.
Katika
shtaka la nne la kughushi, washtakiwa wote walikuwa wakidaiwa kuwa kati
ya Desemba 4, 2010, katika tawi la Bugando, kwa pamoja walitengeneza
nyaraka za uwongo za kuchukulia pesa benki kwa lengo la kufanya
udanganyifu.
Ilidaiwa
kuwa lengo la nyaraka hizo za uwongo lilikuwa ni mteja mmoja aitwaye New
Ana Filling Station, mmiliki wa akaunti namba 01J1016800800, alichukua
pesa kiasi cha Sh 140 miloni katika tawi hilo, jambo ambalo halikiuwa
kweli.
Mshtakiwa wa tatu (Ndaliko) pia alikuwa pia akikabiliwa na shtaka mbadala la kusaidia kutendeka kwa kosa la wizi.
Alidaiwa kuwa kati ya Desemba 4, 2010, na kwa siku nyingine baadaye , akijua kuwa mshtakiwa wa kwanza aliiba pesa jumla ya Sh140 milioni mali ya CRDB, alimsaidia kufuta ushahidi ili kumwezesha kuepuka adhabu.
Shtaka la tano ni la kuwasilisha nyaraka za uwongo, lililokuwa likimkabili mshtakiwa wa kwanza peke yake (Meneja Waijaha).
Alidaiwa kuwa kati ya Desemba 4, 2010, na kwa siku nyingine baadaye , akijua kuwa mshtakiwa wa kwanza aliiba pesa jumla ya Sh140 milioni mali ya CRDB, alimsaidia kufuta ushahidi ili kumwezesha kuepuka adhabu.
Shtaka la tano ni la kuwasilisha nyaraka za uwongo, lililokuwa likimkabili mshtakiwa wa kwanza peke yake (Meneja Waijaha).
Ilidaiwa
kuwa Desemba 4, 2010 katika tawi la CRDB Bugando Mwanza, akijua na kwa
udanganyifu, alitoa risiti ya benki ya kuchukulia pesa kwa lengo la
kuonesha kuwa ilisainiwa na mteja, New Ama Filling Station na akaunti
namba 01J1016800800, jambao ambalo si kweli.
Kwa
mujibu wa maelezo ya awali ya kesi waliyosomewa washtakiwa hao, wizi huo
ulibainika baada ya Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani kumwagiza mkaguzi wa
ndani kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika tawi la Nyanza.
Uamuzi
huo wa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani kuamuru kufanyika kwa ukaguzi wa
kushtukiza katika tawi hilo ulitokana na taarifa zilizopatikana kuwa
kulikuwa na tofauti kubwa ya ulali wa pesa katika tawi hilo.
via gazeti la Tanzania Daima
Alhamisi, Mei 30 mwaka 2013.
Post a Comment