Afisa
mtendaji wa kata ya Iguguno Josia Pangani akizungumzia tukio la
kulawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa wanafunzi wawili wa familia moja
wa shule ya msingi Lukomo wilaya ya Mkalama.
Mama
mzazi wa watoto waliobakwa na kisha kunyongwa hadi kufa Veronica Nuru
mkazi wa kijiji cha Lukomo wilaya ya Mkalama, akizungumzia tukio la
kuuawa kikatili watoto wake.
Makaburi walikozikwa wanafunzi wawili waliolawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Watoto
wawili wa familia moja wameuawa kikatili mkoani Singida baada ya
kulawitiwa na watu wasiojulikana, kisha kunyongwa kabla ya milii yao
kwenda kufungwa kwenye mti porini.
Watoto
hao wametajwa kuwa ni Esta Daudi (14) na Anita Shila (9) wote
wanafunzi wa darasa la saba na tatu katika shule ya msingi Lukomo kata
ya Iguguno wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Afisa
mtendaji wa kata hiyo Josia Pangani, amesema tukio hilo limetokea
majira ya saa 12 jioni wakati watoto hao wa kike wakiwa wanachunga
mifugo kwenye pori jirani na nyumbani kwao.
Pangani
amesema baada ya muda wa kurejesha mifugo zizini kufika, wazazi wa
watoto hao walishangaa kutowaona watoto wala mifugo, hali
iliyosababisha kuanza juhudi za kuwatafuta.
Amesema
juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda siku hiyo hadi kesho yake
walipoikuta miili ya watoto hao ikiwa imefungwa kwenye mti.
Baada
ya uchunguzi wa kitaalamu kufanyika, ilibainika kuwa walibakwa,
kunyongwa shingo, kisha kufungwa vitambaa usoni na watu wasiojulikana.
Habari za kipolisi zinasema kuwa watu wawili akiwemo baba mzazi wa watoto waliouawa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Tukio
hilo limekuja mwezi mmoja tu baada ya mvulana mmoja mkazi wa kijiji
hicho kulawitiwa, kuvunjwa mkono na kutobolewa macho kisha kuuawa, hali
inayozua hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Post a Comment