Msanii
wa muziki wa Kizazi kipya, Ben Paul, atakuwa ni miongoni mwa wakali
watakaoangusha bonge la burudani katika shindano la Redd's Miss Temeke,
Julai 5 mwaka huu.
Wazee wa moja moja, Twanga Pepeta nao pia wataangusha bonge ya burudani katika shindano hilo.
********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
MSHINDI wa tuzo ya utunzi bora wa nyimbo za bongo
fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul amethibitisha na kukamilisha taratibu
zote za kutumbuiza katika shindano la kanda ya Temeke, litakalofanyika Julai 5,
katika ukumbi wa TCC Club Chang’ombe.
Ben Paul ambaye ni kipenzi cha mashabiki warembo kwa
sasa, akiwa na anatamba na nyimbo lukuki zikiwemo Pete, Yatakwisha, Nikikupata
na Waubani, atakuwa sambamba na bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta”,
ambao itakuwa ni mara tu baada ya kuzindua albamu ya 13.
Shindano la Redds Miss Temeke, litakuwa linafanyika
siku chache tu kabla ya mfungo wa Ramadhan, hivyo ni kama vunja jungu kwa wale
wataoingia katika mfungo. Warembo 16 wamekuwa wakiendelea na mazoezi chini ya
wakufunzi Suzan Mwenda na Shadya Mohamed.
Warembo hao ni pamoja na Aksaritha Vedastus ,Irene Rajab, Darline Mmary, Esther
Muswa Hyness Oscar, Latifa Mohamed, Jamila Thomas, Margreth
Rajab, Magdalena Olotu, Mey Karume,Mutesa George, Naima Ramadhan, Narietha
Boniface, Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo.
Mashindano
hayo yamedhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, City Sports
Lounge, Blogu ya Wananchi, RIO Quality Gym &Spa, Fredito Entertainment na
Kitwe General Traders. Temeke,
imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo
na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali.
Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata
kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na
kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili
ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001),
na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya
mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla.
2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo
na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia
kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's
na gazeti la Citizen.
Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika
nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010
alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na
warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania
mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey
mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na
Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds
Miss Temeke.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions
Post a Comment