MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa
na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.
Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba
Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya
Bunge.
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha
Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti
kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.
Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa
Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa
inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
Post a Comment