Askari
kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja
aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T
961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta
jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya
ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika
maeneo ya mabenki.
Askari kanzu akiwa na bastola aliyokamatwa nayo mtu aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.
Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
Pikipiki waliyokuwa wakitumia.
Ofisa
wa Polisi aliyefika katika eneo la tukio akijaribu bastola waliyokutwa
nayo watu wawili waliokuwa katika Pikipiki katika makutano ya barabara
ya Samora na Makunganya, Posta Mpya jirani na Benki ya Bosta leo.
Ngoja niijaribu.
Ofisa wa Polisi aliyefika katika eneo la tukio akiendelea kuikagua.
Mtu aliyekutwa na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa.
Akiwasiliana na ndugu zake.
Akichukuliwa maelezo na Ofisa wa Polisi.
Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabila gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji dereva wa pikipiki.
Post a Comment