KIBO EXECUTIVE LODGE ILIYOPIGWA MNADA |
Mambo yamezidi kumwendea vibaya Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Vicky Swai (pichani) kutokana na hoteli yake yenye ghorofa moja kuuzwa kwa mnada kwa Sh600 milioni.
Hoteli hiyo iliyopo kiwanja namba 89 eneo la
Shanty Town mjini Moshi inayofahamika kama Kibo Executive Lodge, iliuzwa
mwishoni mwa wiki ili kufidia deni la Sh350 milioni anazodaiwa na Benki
ya CRDB.
Mnada wa kuuza hoteli yake hiyo ulifanyika
Jumamosi iliyopita, ukiendeshwa na Kampuni ya Madalali ya Comrade
Auction Mart Co Ltd ya jijini Dar es Salaam iliyopewa idhini hiyo na
Benki ya CRDB.
Kabla ya kufanyika kwa mnada huo, madalali hao
walitoa matangazo katika magazeti ya Daily News na Uhuru ya Mei 17,2013,
wakiujulisha umma kuwa baada ya siku 14 wangeiuza hoteli hiyo.
Kampuni ya Charan Singh and Sons Ltd kupitia kwa
mwakilishi wake, Agustino Rafael Mrema ndiyo iliyotoa ofa ya juu zaidi
ya Sh600 milioni ambayo haikuweza kufikiwa na mnunuzi mwingine yeyote.
Swai amekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro
kwa vipindi viwili mfululizo (2004-2008 na 2008-2012) na kabla ya
hapo,alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Jumuiya ya Wanawake (UWT).
Mwaka jana hakutetea wadhifa wake huo lakini
akagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kupitia
Wilaya ya Hai Mkoa Kilimanjaro, lakini kamati kuu haikurudisha jina
lake.
Post a Comment