Baadhi ya
majeruhi wa mlipuko wa bomu lililotokea mwishoni mwa wiki mjini
Arusha.
ARUSHA,
Tanzania
IDADI ya
watu waliokufa kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki wakati
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiwa katika mkutano wa kampeni za
udiwani katika Kata ya Soweto mjini Arusha imefikia watatu.
Akitoa
taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mlongo amesema kuwa idadi hiyo
imeongezeka baada ya majeruhi mmoja kufariki wakati akipata matibabu na majeruhi
wengine bado wanaendelea na matibabu.
Tukio hilo
limetokea wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani mkoani
Arusha.
Wakati
idadi ya vifo ikiongezeka hali ya majeruhi wengine si nzuri na wamekimbizwa
nchini Kenya kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi amesema kuwa
mtu hatakayefanikisha kupatikana kwa aliyehusika na tukio hilo atapata zwadi ya
sh. milioni 100.
Akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo, Mh. Lukuvi
amesema kuwa serikali itatoa zawadi ya sh. milioni 100 kwa mtu
atakayefanikisha kupatikana kwa mtu aliyehusika katika mlipuko wa bomu katika
Kata ya Soweto mjini Arusha ambapo mkutano wa
hadhara wa kampeni za udiwani zilikuwa zikifanyika.
Post a Comment