Kinyanganyiro
cha kumtafuta mnyange wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa
usiku wa ijumaa baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha
mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 13 waliojitokeza.
Nyota
ya mrembo huyo ilianza kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa,
lakini zaidi aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika
ukumbi wa Yatch club baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni
changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watawakilisha mkoa wa mwanza katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu.
Post a Comment