Mohamed
Gwalima enzi za uhai wake kulia akijiandaa kumzawadia Kompyuta
aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka wakati wa
hafla ya kumuaga iliyofanyika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa ,wa
pili kulia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Joseph Muhumba na
mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita. (Picha na Francis Godwin
Blog)
" Ni kweli ndugu mwandishi habari hizo ni za kweli kabisa nimepigiwa simu na mganga mkuu wa wilaya ya Kilolo juu ya kifo hicho"
Mfanyabiashara
maarufu mkoani Iringa na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Salim Abri
Asas (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye
thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 3.2 kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw.
Gerald Guninita hivi karibuni ofisini kwake wanaoshuhudia ni mwenyekiti
wa Halmashauri ya Kilolo Joseph Mhumba, kushoto na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kilolo Momahend Gwalima ambae ni marehemu sasa.
Waombolezaji
wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wilaya ya
Kilolo Mohamed Gwalima. (Picha na Francis Godwin
Na Francis Godwin, Iringa
ALIYEKUWA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa,
Mohamed Gwalima afariki dunia ghafla nyumbani kwake Kilolo.
Akithibitisha
kutokea kwa kifo cha Mkurugenzi huyo Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald
Guninita ambae yupo kikazi mjini Dodoma amesema kuwa mkurugenzi huyo
amefariki ghafla nyumbani kwake baada ya kuwasili kutoka safari jijini
Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alipigiwa simu kujulishwa juu ya kifo cha mkurugenzi huyo usiku huu.
" Ni kweli ndugu mwandishi habari hizo ni za kweli kabisa nimepigiwa simu na mganga mkuu wa wilaya ya Kilolo juu ya kifo hicho"
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Joseph
Muhumba alisema kuwa kifo cha mkurugenzi huyo kimeacha pigo kubwa
katika Halmashauri ya Kilolo.
Kwani alisema kabla ya kifo cha ghafla cha mkurugenzi huyo alikuwa nae
jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta wahisani wa kusaidia kufufua
kiwanda cha Chai kidabaga ili kuwakomboa wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa mbali ya kuwa kifo hicho kimetokea ghafla ila mkurugenzi
huyo kabla ya kifo chake alikuwa akilalamika kusumbuliwa na tatizo la
Kisukari .
Muhumba alisema kuwa kifo cha
mkurugenzi huyo kilitokea ghafla usiku wa kuamkia leo baada ya kurejea
kutoka jijini Dar es Salaam ,pia amewapa pore nyingi wananchi wa Kilolo
kwa msiba huo mzito.
Wakati
huo huo waombolezaji walifika kuaga mwili wa mkurugenzi huyo
walieleza kusikitishwa kwao na hatua ya kamati ya mazishi kushindwa
kutoa nafasi kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilolo na Halmashauri
nyingine mkoa wa Iringa pamoja na wananchi kuaga mwili huo.
Mbali
ya waombolezaji hao zaidi ya 500 kufika mapema zaidi katika viwanja vya
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
kwa ajili ya kuaga mwili huo ila hali imekuwa tofauti baada ya kuwepo
kwa ratiba zinazochanganya zaidi ya mbili.
Taarifa
za awali zilizotolewa zilionyesha kuwa mwili huo ungeagwa majira ya saa
4 asubuhi ila baadhi ya watu waliofika mida hiyo kuaga waliambiwa kuwa
mwili huo ungeagwa mida ya saa 7 mchana na baada ya kufika majira ya saa
7 mchana lilitolewa tangazo jingine na kaimu mkurugenzi kuwa taratibu
za kuuandaa mwili zinaendelea na mara baada ya kuaga basi mwili huo
utapelekwa msikitini .
Hata
hivyo hali haikuwa hivyo wananchi waliokuwa wamejiandaa kwa ajili ya
kuaga mwili huo walijikuta wakiduwaa baada ya mwili huo kutolewa chumba
cha maiti na kupakiwa katika gari kisha kupelekwa msikitini na baada ya
msikitini mwili huo uliingizwa katika gari jingine la wagonjwa na
kuondoka kuelekea kijiji cha Ikwiriri Rufiji kwa mazishi yatakayo
fanyika kesho.
Baadhi ya watumishi waliofika kuaga mwili huo wameonyesha kusikitishwa na hatua ya kutouaga mwili wa mkurugenzi wao,
marehemu
alizaliwa tarehe 16 februari 1957 ikwiriri rufiji na kupata elimu ya
sekondari kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne katika shule ya
sekondari same kuanzia mwaka 1978-1980 alipata elimu ya kidato cha tano
na sita katika shule ya sekondari shinyanga
mwaka
1980 mpaka 1981 alitumikia taifa katika jeshi la kujenga taifa kabla ya
kujiunga na masomo ya shahada ya uchumi katika chuo kikuu cha dar es
salaam,stashahada aliyotunukiwa mwaka 1986
Mara baada ya kutunukiwa shahada ya uchum i mwaka 1986,aliajiriwa kama mchumi katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara.
Al;itumikia
taifa katika maeneo mbalimbali kama mchumi mpaka mwaka 2007
alipoteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya
Mbulu.
Mwaka
2012 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya Mtwara na mwaka huu
2013 alihamishiwa katika halimashauri ya wilaya ya kilolo ambako amekuwa
mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo mpaka mauti ilipo mfika tarehe
25/06/2013 saa 1:15 jioni katika nyumba aliyokuwa anaishi na familia
yake ilyopo karibu na ofisi za halimashauri hiyo.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA
Post a Comment