Meza kuu
Lango la kuingilia chuoni
hapo
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa(M-NEC) Mbunge
Jimbo la Monduli, akiwa anaingia katika kanisa la Moravian Tanzania usharika wa
Ruanda Jijini Mbeya 25.11.2012. kuchangia chuo cha TEKU (Picha na maktaba ya
kalulunga
Na Gordon Kalulunga, Mbeya
WAHADHILI wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Mbeya kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania, wameitaka serikali na
mamlaka zinazosimamia vyuo vikuu nchini, kuchunguza taaluma za wahitimu wa chuo
hicho.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, walisema
kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya wanafunzi wanaofeli masomo na
kutakiwa kurudia, wakiongezewa alama za ufaulu huku wakufunzi wasio na sifa
wakizidi kuajiliwa.
Walisema kutokana na hali hiyo, hawatatunga mitihani
ya mhula iliyotarajiwa kuanza Julai 1, mwaka huu kutokana na kupuuzwa na utawala
wanapotoa ushauri wa kitaaluma.
Kaimu Mwenyekiti wa chama cha wahadhili wa chuo hicho
(TEKUASA), Amani Simbeye, alisema wahadhili hao zaidi ya 42 walifikia hatua ya
kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kutokana na kupewa kauli za
vitisho na matusi wanapohoji au kushauri mambo
kitaaluma.
‘’Kutokana na hali hiyo hatuna imani na makamu mkuu
wa chuo, maana utawala unafanya mambo yote bila kushirikisha wahadhili ikiwemo
kupunguza muda wa masomo kwa wiki mbili na kusababisha walimu kushindwa kumaliza
mada na tumeshushwa morali ya kazi’’ alisema Simbeye.
Aidha alisema kutokana na uongozi wa chuo kufanya
mambo bila kuzingatia utawala bora na kuheshimu wahadhili, imefikia hatua
wanafunzi hufaulishwa kwa kupewa alama za ufaulu katika masomo wanayofeli
akiwemo mwanafunzi Mbunda Samson ambaye amefaulishwa na uongozi umeshindwa
kutolea ufafanuzi jambo hilo.
Wahadhili hao walisema mbali na hayo, kuna ukosefu wa
idara za masomo ikiwemo watu wa kusimamia ubora wa taaluma itolewayo na
chuo,hali waliyoitaja kuwa ni uasi wa waumini wa kanisa la Moravian Tanzania
wanaotoa sadaka na kuchangia harambee kukiwezesha chuo
kuendelea.
‘’Tumekaa kimya kwa muda mrefu na lengo letu ni kuokoa
chuo na taaluma itolewayo hapa chuoni’’ alisema
Simbeye.
Makamu mkuu wa chuo hicho Prof. Tuli Kasimoto
hakupatikana chuoni hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa nje ya mkoa wa
Mbeya.
Kaimu Makamu mkuu wa chuo hicho Dr. Daniel Mosses,
alipofuatwa ofisini kwake ili kuweza kujibu tuhuma hizo, alikataa kuzungumzia
suala hilo kwa madai kuwa yeye siyo msemaji.
Novemba 25, 2012, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa
alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia chuo hicho cha TEKU ambapo
alitoa Shilingi Milioni 10 katika sherehe zilizofanyika katika kanisa la
Moravian Tanzania usharika wa Ruanda mjini Mbeya.
Hata hivyo, uchunguzi umebaii kuwa mgogoro kati ya
wahadhili hao na uongozi wa chuo hicho umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja ambapo
imefikia hatua baadhi ya wahadhili wamekataa uteuzi wa vyeo vya juu vya chuo
hicho licha ya kuahidiwa mishahara minono huku wengine saba wakidaiwa kung’atuka
kwenye nafasi zao za idara.
Post a Comment