Na Belinda Kweka- MAELEZO
CHUO
Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili(MUHAS) kipo katika mpango wa
kujenga chuo kipya kwa ajili ya ufanyaji mazoezi kwa wanafunzi.
Ujenzi
huo unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika eneo la Mloganzila
Kibamba ambapo , ukimalizika utachukua wanafunzi 15,000 watakaosoma
taaluma mbalimbali za afya.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere
jijini Dares Salaam (sabasaba) ,Afisa Mipango Mkuu wa chuo hicho
Ulimbaga Kijobile alisema uamuzi huo umetokana na ongezeko la
wanafunzi ni wengi.
Alisema
eneo hilo lita wezesha wanafunzi hao kupata sehemu za kusomea kwa
ufanisi kama vile ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za
ufanyaji mazoezi.
“Tumeamua
kuanzisha mradi kwa kujenga chuo kipya kwa sababu MUHAS ina sehemu
ndogo na hatuwezi kuipanua kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa chuo ili
kuweza kutosha kwa wanafunzi” alisema Kajobile.
Aidha
alisema wanafunzi hao , walikuwa wakipata tabu katika kufanya mazoezi
,hivyo hulazimika kwenda hospitali za Mwananyamala na Amana.
“Muda
mwingine tunatumia hospitali nyingine ili kupata sehemu ya kutosha
lakini hospitali hii itakayojengwa itasaidia kuchukua wanafunzi wote ili
kuweza kufanya mazoezi yao bila usumbufu” alisisitiza Ulimbaga.
Alisema
ujenzi wa chuo hicho, kinakadiriwa kujengwa ndani ya mwaka
mmoja,ambapo wanafunzi wa muhula wa kwanza wa mwaka 2015 wanatarajiwa
kuanza.
Aliongeza
kuwa kitatoa huduma za kiafya kama hospitali nyingine hivyo wananchi
wa eneo hilo wanashauriwa kufika mara baada ya ufunguzi wa chuo hicho
ili kupata matibabu mbalimbali.
Post a Comment