Mwenyikiti wa timu ya Maji Maji Humphery
Millanzi aliyeibuka kidedea kwa ushindi mkubwa katika uchagui wa viongozi wa
timu hiyo.
..........................
Na Amon
Mtega
,Songea.
TIMU ya majimaji ya wanalizombe mkoani Ruvuma jana
imepata uongozi mpya utakao weza kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka
minne.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ,Joseph
Mapunda uliyofanyika katika ukumbi wa saccos ya walimu uliyopo mjini hapo
alisema kuwa kwa nafasi ya mwenyekiti imechukuliwa na Humphery Millanzi
kwa kura 89 huku mpinzani wake Mohamed Issa alipata kura
30.
Mapunda alisema kuwa kwa nafasi ya makamu mwenyekiti
mgombea alikuwa ni John Nchimbi ambaye alikuwa mgombea peke bila
upinzani na kufanya apate kura za ndiyo 101huku kura 20 zilikuwa za
hapana.
Akifafanua katika nafasi za wajumbe watano alisema
kuwa nafasi hizo ziliwaniwa na watu tisa waliyopatikana ni watano nao ni Hilda
Kapinga alipata kura 102 Mohamed Matwika kura 99 John Kabisama kura 90
Kitwana Mzee kura 84 na Salum Masamaki kura 74
.
Aidha alisema kuwa kwa wajumbe walishindwa kupata
nafasi hizo ni Joseph Mswila ambaye alipata kura 62 Robarti Mgowole kura 18 Said
Mangwe kura 14 na Oddo Mbunda kura 50 huku idadi ya wapiga kura walikuwa
121.
Kwa upande wake mwenyekiti aliyeshinda katika nafasi
hiyo Hafrei Milanzi akiongea na chombo hiki alisema kuwa amepongeza ushindi huo
huku akiwa ameahidi kushirikiana na wanachama wote wa timu ya majimaji pamoja na
wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kusongambele kimchezo.
MWISHO.
Post a Comment