Mlinda Mlango Deogratius Mushi 'Dida' akifanya mazoezi
na wachezaji wenzake wa Yanga, Loyola Sekondari hii leo.
KIPA mpya aliyesajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Deogratius Munishi 'Dida' pamoja beki wa kati
aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Rajab Zahir leo wameanza rasmi
mazoezi na timu yao Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es
Salaam.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema jana katika siku ya kwanza ya mazoezi kiungo
mshambuliiaji Mrisho Khalfan Ngassa alifanya mazoezi asubuhi chini ya kocha
mholanzi Ernest Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi wachezaji wote wa timu
ya taifa, Taifa Stars kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo dhidi ya Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Hadi sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji
watano wapya ambao ni Dida kutoka Azam, Zahir wa Mtibwa, Ngassa wa Simba, Shaban
Kondo aliyekuwa Msumbiji na Realitus Lusajo kutoka Machava
FC.
Kocha Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji hao
kwani amesema atapata fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki kanda ya
ziwa hali itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na msimu mpya
wa 2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi Loyola ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya ziara yake Kanda Ziwa inayotazamiwa kuanza mwishoni
mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezaji wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda.
Via/www.mrokim.blogspot.com
Post a Comment