Na Mahmoud Zubeiry, wa Bin Zubeiry
HATIMAYE
mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’
amesaini Mkataba wa miaka miwili usiku huu kuendelea kuichezea klabu ya
Yanga SC ya Dar es Salaam.
Majemedari watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.
Majemedari watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.
Kiiza alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam majira ya Saa 12 jioni na moja kwa moja kwenda kumalizana na Yanga.
Hii ilikuwa mara ya tano, Kiiza anakuja Dar es Salaam kwa ajili ya suala la kusaini Mkataba na mara nne zote za awali, alishindwa kuafikiana na uongozi wa klabu hiyo akarejea Uganda, mara ya mwisho ikiwa ni wiki iliyopita.
Awali, mara tu baada ya Ligi Kuu, Yanga ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, hawakufikika makubaliano akaondoka. Mara ya pili, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro akapanda ndege Uganda kuzungumza naye, wakafikia makubaliano akamtumia tiketi aende Dar es Salaam.
Hata hivyo, mpachika mabao huyo alipofika Dar es Salaam akaona kama anapotezewa muda, kwa sababu Yanga ilionekana kutegeshea matokeo ya majaribio ya mshambuliaji kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi, akifuzu imteme Kiiza, na Mganda huyo akapanda ndege kurejea Kampala.
Yanga SC baada ya kugundua Chukwudi ni majeruhi wa muda mrefu, ikamtumia tiketi Kiiza mwishoni mwa mwezi uliopita arejee tena Dar es Salaam, lakini pia akapanda ndege kurejea Uganda, bila kusaini Mkataba.
Tayari mshambuliaji Mnigeria, Ogbu Brendan Chukwudi amerejeshwa kwao baada ya kuonekana ni majeruhi sugu.
Kwa kusaini Yanga, Kiiza anakuwa mchezaji wa nne katika orodha ya wachezaji wa kigeni baada ya beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, hivyo klabu itabakiza nafasi moja.
Yanga SC sasa inaendeleza mapambana yake na watani Simba SC katika kuwania saini ya Mganda mwingine, Moses Oloya ambaye anamaliza Mkataba wake na Saigon Xuan Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti.
Post a Comment