Na Anna Nkinda – Maelezo
Wanawake
nchini wametakiwa kuishi maisha ya upendo, umoja na mshikamano bila ya
kuangalia itikadi zao za dini na vyama vya siasa hatua itakayosaidia
kuimarisha hali ya amani na utulivu.
Wito
huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa futari
ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wanawake viongozi na wake wa
viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam .
Mama
Kikwete alisema hakuna dini hata moja inayowafundisha watu kuishi
maisha ya chuki bali dini zote zinasisitiza kuishi kwa amani, umoja, na
upendo jambo ambalo litamfanya binadamu aweze kumfikia Mwenyezi Mungu.
“Bila
ya kuangalia itikadi zetu tulizonazo, sisi kama viongozi na wake wa
viongozi tutumie nafasi tuliyonayo kuzungumza kwa vitendo maneno matatu
ya upendo, amani na mshikamo ili jamii yetu iweze kuiga mfano kutoka
kwetu”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia
ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Rose Migiro
alimshukuru Mama Kikwete kwa ajili ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao
ambayo imewafanya waweze kukutana kwa pamoja na kuweza kubadilishana
mawazo.
Dk.
Migiro alisema kuwa hivi sasa watu wote wanatakiwa kuliombea taifa
amani na salama pia Mwenyezi Mungu awajalie viongozi wote busara, afya
njema na mshikamoano ili waweze kuongoza watu vizuri na kwa amani.
Post a Comment