Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAHIMIZA WANANCHI KUJIKITA KATIKA UFUGAJI NYUKI

 

asal 2
Naibu Waziri wa Maendeleao ya Mifugio na Uvuvi, Mhe. Benedict Ole Nangoro (MB) (mwenye suti) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka kikundi cha SULEDO.
………………………………………………………………………….
Serikali imeimiza wananchi kujikita katika miradi ya ufugaji nyuki inayohitaji uwekezaji mdogo na faida kubwa ili kufikia lengo la kuwa na maisha bora kwa kila mtanzania.
Rai hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Maendeleao ya Mifugio na Uvuvi, Mhe. Benedict Ole Nangoro (MB) muda mfupi kabla ya kuzindua mashindano ya Mifugo na Maonesho ya Ufugaji Nyuki Kitaifa mwaka huu katika Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Nzuguni mjini Dodoma.
Mhe. Nangoro alisema shughuli za ufugaji nyuki ni nzuri na endelevu kutokana na kutohitaji mtaji mkubwa wakuanzia na hata uvunaji, usindikaji wa asali na mazao mengine yatokanayo na nyuki hutumia tekinologia rahisi
“Utunzaji ama ufugaji nyuki ni shughuli inayomwezesha mwananchi kupata kipato cha kutosha bila kuwekeza mtaji mkubwa lakini pia tekinolojia yake ni rahisi kwani haina madai ya ajabu ajabu,” alisema Mhe. Naibu Waziri.

Mhe. Nangoro alisema shughuli za ufugaji nyuki ni eneo lingine ambalo watu wakielekeza ujasiriamali wao watanufaika bila madai makubwa na hivyo kujiongezea kipato katika kaya, kuchangia lishe, tiba, uboreshaji wa mazingira na utunzaji wa habitanti inayohitajika na nyuki kuzalisha asali.
Aidha, Mhe. Naibu Waziri na vingozi waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii walipata fursa ya kutembelea Mradi wa Ufugaji Nyuki wa Chama cha Ushirika cha Huduma, Mtandao wa Askari wa kike Tanzania wilayani Chamwino kujionea shughuli mbalimbali za kikundi hicho.
Akielezea mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Bi. Fatma Ally alisema, walianzisha mradi huo mwezi Oktoba 2012 ili kupata fedha za kuendesha huduma kwa akina mama na watoto wanaofanyiwa ukatili na unyanyasaji wa kimwili, kiuchumi na kiakili
Alisema mradi huo una jumla ya mizinga 543 yenye uwezo wa kuzalisha wastani wa lita 5000 za asali zenye thamani ya tshs 50, 000, 00/= kwa mwaka.
Aidha, alisema wanatarajia mradi huo kutumika kama shamba darasa kanda ya kati na kuwa na mizinga zaidi ya 1000 ifikapo Desemba 2013; na kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vingine vya ufugaji nyuki ndani na nje ya mkoa wa Dodoma.
Kufuatia mafanikio ya kikundi hicho, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu ilitoa mizinga 10 kwa wanakikundi hao.
Akitoa mizinga hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Nuru Millao alisema Wizara imefarijika na mafanikio ya wanakikundi na hivyo imeamua kuwapa mizinga 10 ili waweze kufikia malengo ya kutimiza mizinga 1000.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleao ya Mifugio na Uvuvi, Mhe. Benedict Ole Nangoro (MB) aliwataka wanakikundi hao kuzingatia nidhamu kwenye kundi, kutunza mazingira ili waweze kupata asali yakutosha na kuepuka kulina asali kabla haijaiva.
Sherehe za Nane Nane zinafanyika Kitaifa mjini Dodoma katika Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Nzuguni uliopo kilomita saba kandokando mwa barabara ya Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kauli mbio ya sherehe hizi mwaka huu ni “zalisha mazao ya kilimo na mifugo kwa kulenga mahitaji ya soko”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top