Kila mwananchi wa Zanzibar ameshitushwa na kusikitishwa na tukio la
kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku tareh 7 Agost
2013 huko katika maeneo ya Mji mkongwe Zanzibar yaliopo mahoteli mengi
na makazi ya wageni wanaotembele nchi yetu kutoka sehemu mbali mbali
duniani.
Chama Cha wananchi CUF kinalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili
la kuwamwagia tindi kwa wageni wetu hao,na kinalitaka Jeshi la Polisi
Zanzibar kufanya uchunguzi wakina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa
wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Matokeo haya ya kikatili ya kumwagiwa kwa watu tindi kali yamekuwa
yakishamiri siku hadi siku ndani ya visiwa vya Zanzibar,ambayo yamekuwa
yamewathiri watu kadhaa tena bila ya wahusika kuweza kupatikana na
kuchukuliwa hatuwa za kisheria kiasi ambacho sasa jamii ya wazanzibar
imejengeka katika hofu juu ya usalama wa maisha yao ya kila siku,Hii ni
dalili mbaya kwa Nchi ya Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali
yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia
uchumi wa Visiwa vyetu.
Kufanyiwa hujuma raia hao wakike wawili wa kigeni kutoka nchini
Uengereza kigeni ambao walikuwa Zanzibar kwa kazi za kujitolea
(valantia) kusomesha katika skuli za msingi (primary)
ni dhahiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.
ni dhahiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.
Chama cha wananchi CUF kinawataka wananchi wote wa Zanzibar kutoa kila
aina ya mashirikiano ya kuweza kufanikisha kukamatwa wahalifu hao na
hatimae kufikishwa katika sehemu husika.
Sambamba na hilo Chama cha wananchi CUF Kinawataka Wanachi wote, Polisi
jamii kutoa kila aina ya mashirikiano kwa Jeshi la Polisi ili jeshi hilo
liweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi yetu,
kwa lengo la kuiendeleza sifa ya asili ya zanzibar isemayo kuwa
Zanzibar ni njema atakae na aje…
Haki sawa kwa wote.
Salim A Biman
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma
Post a Comment