Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DAKTARI WA RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE, PROFESA JANABI AINGIA KUNDI DOGO LA MADAKTARI WA AFRIKA WALIOTHIBITISHA KUWA NA UJUZI NA UTAALAM WA KUWAPIMA NA KUTOA LISENI ZA VIPIMO VYA AFYA KWA WATUMIANJI WA ANGA


Profesa Mohammed Y. Janabi (pichani) , Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanikiwa kuingia katika kundi dogo la madaktari wa Afrika waliothibitisha kuwa na ujuzi na utaalam wa kuwapima na kutoa liseni za vipimo vya afya kwa watumishi wa anga wakiwamo marubani.
Katika barua ambayo aliipokea Dkt. Janabi wakati anaandamana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya Marekani na Canada iliyomalizika leo, Jumamosi, Septemba 28, 2013, Wizara ya Usafirishaji ya Marekani kupitia Utawala wa Shughuli za Anga wa Marekani (FAA) imesema kuwa imemteua Profesa na Dkt. Janabi kuwa Daktari wa Shughuli za Anga (AME)
kuanzia Agosti 14, mwaka huu, 2013.
“Uamuzi huu una maana
kuwa sasa unaweza kuwapima na kuendesha shughuli za kitibabu na kutoa ama
kukataa kutoa liseni ya kuthibtisha afya za watumishi wa sekta ya anga wakiwemo
marubani wa ndege za usafirishaji, wa ndege za biashara za abiria, marubani wa
ndege binafsi na marubani wanafunzi.
Profesa Janabi
anakuwa daktari wa 31 katika Afrika na wa tatu katika Afrika Mashariki kupatiwa
hadhi hiyo ambayo inapatikana baada ya kazi ngumu ambayo ni pamoja na kufanya
mtihani maalum.
Nchi pekee katika
Afrika Mashariki iliyokuwa na madaktari wa kiwango hicho kabla ya Dkt. Janabi
kuingia katika kundi hilo ni Kenya yenye madaktari wawili. Tanzania sasa
inakuwa nchi ya pili katika Afrika Mashariki kuwa na hadhi hiyo.
Kwa upande wa Afrika,
Profesa Janabi anaungana na madaktari kutoka Burkina Faso (1), Cameroun (2),
Misri (6) ambayo ndiyo madaktari wengi zaidi katika kundi hili, Ghana (1),
Libya (1), Morocco (1), Nigeria (5), Ethiopia (4), Kenya (2), Afrika Kusini (5)
kukubaliwa kuifanya kazi hii ya kimataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 29
Septemba, 2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top