Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia
waimbaji wa kwaya mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nyashimo
Wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu, Ndugu Abdulrahman Kinana
amemaliza ziara yake kwenye mkoa huo ambapo amekagua miradi ya maendeleo
na kuzungumza na wenyeviti wa mashina pamoja na wanachama wa CCM ili
kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi
katika maeneo mbalimbali moani humo, Kinana anaaza Ziara ya siku sita
katika mkoa wa Mara. Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo
uliofanyika mjini Lamadi Busega Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa
Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasiapamoja
na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha
wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili
kumaliza tatizo la malimbikizo hayo, Kinana amesema kama watendaji hao
wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki
kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya
Kikwete ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu,
Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya
na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus
Kamani. (PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LAMADI SIMIYU)
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC
Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakifurahia ngoma za akina
mama walipowasili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi
pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha bodaboda wa Nyashimo
Gasper Mabula
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimnawisha
mikono Mwenyekiti wa shina Sina namba 1 kijiji cha cha Nyamatembe Bi.
Sophia Kayenze tayari kwa kupata kifungua kinywa cha chai kwa Michembe .
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika kijiji cha Nyamatembe.
Nape
Nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na
wananyamitembe mara baada ya kuwasili kijijini hapo wakitokea Bariadi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kama
mshauri mkuu wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dr. Jakaya Kikwete katika kijiji cha Mwamanyiri mahari ambapo
Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. nyerere alipumzika na kulala akitokea
Butiama kwenda Mwanza wakati akiunga mkono Azimio la Arusha mwaka 1967.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kujenga ofisi ya Chama cha Mapinduzi kata ya Mwamanyiri huku Nape Nnauye
akimsaidia kumpati tofari.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kata ya kabita wilayani Besega.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi
pikipiki kwa mwenyekiti wa kikundi cha waendesha Lamadi Busega bodaboda Doto Paulo .
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti kulia akizungumza jambo na Mkuu
wa wilaya ya Besega Paul Mzindakaya kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Lamadi Busega.
Kikundi cha ngoma cha lamadi Busega kikitumbuiza katika mkutano huo.
Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara wakifuatilia matukio ya mkutano huo.
Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akuhutubia wananchi
katika mkutano huo wa hadhara mjini Lamadi wilayani Busega.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi Simiyu.
Post a Comment