Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Penina Mlama
kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kipindi cha
miaka mitatu ijayo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari - MAELEZO leo, Uteuzi
huo wa Profesa Mlama unanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka
2016.
Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka
mitatu ijayo kuanzia mwaka huu.
Walioteuliwa
ni pamoja na wawakilishi w
a Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo
ambao ni Dkt. Vincensia Shule, John Kitime , Angela Ngowi, Dkt. Herbert
Makoye, Erick Shigongo na Alex Msama.
Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce Fisoo.
Wanaoingia kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa BASATA.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Kabla ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa.
Wajumbe
wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye,
Prof. Emanuel Mbogo, Dkt. Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na
Katibu Mtendaji wa BASATA.
Wakati
huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza la Kiswahili
la Taifa (BAKITA) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013 hadi
2015.
Wajumbe hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa, Dkt. Issa Zidi, Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.
Wengine
ni Mmanga Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth
Konga, Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.
Wajumbe wengine ni Ally Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin Mgendera.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la BAKITA atachaguliwa na
wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha kwanza.
Post a Comment