RAIS
Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya chakula
cha jioni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakunga kwenda
kusoma ili kupunguza vifo vya mama na mtoto, Oktoba 11, mwaka huu.
Kwa
mujibu Meneja wa shughuli hiyo wa Kampuni ya Montage Ltd, Michael
Philipo alibainisha kuwa maandalizi ya harambee hiyo yameshakamilika na
tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali nchini.
Philipo
alisema Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi hasa kutokana na juhudi zake
za kupambana na vifo vya akina mama watoto nchini, katika harambee hiyo
itakayofanyika hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.
“Kampuni
ya Montage kwa kushirikiana Taasisi ya Utafiti wa Dawa Afrika (AMREF),
kwa pamoja na wadau wengine tutashirikiana kwa pamoja ilikuokoa
wanawake na watoto hasa sehemu mbalimbali za nchi yetu” alisema Philipo.
Na
kuongeza kuwa, wanatarajia kupata watu 450 kwenye harambee hiyo
ambapo tiketi hiyo moja inapatikana kwa dola 150 na tiketi ya meza moja
yenye viti 10, ikipatikana kwa dola 1500.
Aidha,
alitoa rai kwa kila mtanzania kujitokeza kuchangia kwani fedha hizo
zitawasaidia kusomesha wakunga hao wa jadi ambao wataisaidia jamii nzima
nchini kote
Post a Comment