KITUO CHA UWEKEZAJI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Kituo
cha Uwekezaji Tanzania TIC kinapenda kutoa taarifa kwa Umma kuhusu
mafanikio ya Mpango wa kuwaunganisha Wajasiriamali wadogo na wakati
(Business Linkage)na Makampuni Makubwa ya kigeni (TNC’S) na ya
Kitanzania ambapo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo na Biashara (UNCTAD) Mpango huo wa kukuza Uwezo wa kibiashara
kwa wajasiriamali kufanya biashara na Makampuni hayo makubwa.
Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni moja Taasisi ya Serikali ilianzishwa
chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Namba 26 ya mwaka 1997 kwa
kuendeleza, kuratibu na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania. Kama sehemu
ya jukumu letu, TIC ina jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala
yanayohusiana na Uwekezaji kwa Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na
manufaa kwa Watanzania kwa ujumla.
Katika
kipindi chote cha Mpango huo Watanzania wameweza kuongezewa uwezo kwa
kupewa fursa mbalimbali za kiutalamu za kuweza kukabiliana na ushindani
na kuwawezesha kufikia viwango vya Kimataifa vinavyohitajika na
makampuni makubwa ili Makampuni hayo yaweze kutumia bidhaa za Kitanzania
badala ya Kuagiza nje Bidhaa hizo.
Mpaka
sasa kituo kimeweza kutoa mafunzo hayo ya Kitaalamu kwa WAJASILIAMALI
wapatao 285 katika mikoa ya Dar-es-salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.
Katika Mafunzo hayo zaidi ya MAKAMPUNI MAKUBWA 28 yaliweza kuhusishwa katika kuwajengea uwezo na kuwaongezea Utaalamu.
TIC
pia katika jitihada zake za kuongeza faida za uwekezaji katika uchumi
wa Tanzania pia walifanya shughuli kuu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha
wawekezaji kupata vibali vyote vinavyohitajika chini ya One Stop Shop na
utoaji wa huduma kwa wawekezaji aftercare.
TIC
imeweza kusajili Miradi kadhaa na katika usajili huo inawasilisha sekta
tano zinazoongoza katika kusajiliwa miradi katika kipindi cha Januari
mpaka Juni 2013 ambazo ni sekta ya Uzalishaji viwandani miradi 138,
Utalii miradi 115, Usafirishaji miradi 82 majengo ya biashara miradi 65
na kilimo miradi 23. Jumla ya miradi yote ilikuwa ni miradi 454 na
matarajio yetu ni kuwa mwaka huu tutasajili miradi zaidi.
Katika
usajili wa miradi hiyo wawekezaji wa nje waliweza kusajili miradi 120 ,
Miradi ya Ubia kati ya wageni na watanzania ilikuwa ni 92 na miradi ya
Watanzania 242 ambayo ni zaidi ya nusu ya miradi yote.
Post a Comment