********
Singapore. Baadhi ya wabunge ambao wapo ziara ya mafunzo ya
uendelezaji makazi nchini Singapore, wamesema wamechoshwa na ziara za
aina hiyo, huku wakiitaka Serikali kutekeleza yale ambayo wamekuwa
wakiyaona nje ya nchi.
Wabunge hao walitoa kauli hizo jana baada ya
kutembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Uendelezaji Miji ya Singapore
(Ura), ambako walielezwa jinsi mamlaka hiyo inavyosimamia sheria za
mipango na uendelezaji miji.
Ziara hiyo ambayo pia inamshirikisha Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye, kumekuwa
na mjadala mkali kuhusu namna miji ya Tanzania isivyo na mpagilio,
matumuzi ya ardhi yasiyo na tija na mipango isiyozingatia vipaumbele vya
nchi.
Mbunge wa Magomeni (CCM), Mohammed Chomboh
alisema: “Kinachoniumiza moyo ni kwamba tutakuwa si watendaji na
tunabaki wasemaji na wapangaji hadi lini? Natoka Zanzibar, kiongozi wetu
wa kwanza Mzee Abeid Amaan Karume aliamua tu kwamba tunataka nyumba za
wananchi wetu za kisasa na tunaweza na akafanya”.
Hata hivyo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema),
alisema ni vigumu kwa NHC kumudu kutekeleza majukumu yake kwa manufaa
ya umma kwani shirika hilo halipewi ruzuku yoyote kutoka Serikalini.
Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF),
alisema tatizo kubwa ni uongozi ambao umeshindwa kuleta mabadiliko na
kwamba, demokrasia imekuwa ikitumika kama kigezo cha kulea uozo katika
utendaji.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali, Zitto Kabwe, alisema wakati mwingine wabunge wamekuwa wakiona
aibu kuendelea kujifunza kila kukicha na kwamba, lazima ifike mahali
itoshe ili kuilazimisha Serikali kuingia kwenye utekelezaji.
“Jambo la msingi kwa wabunge ni kwenda kusisitiza mambo haya ndani ya Bunge,” alisema Zitto.
kama NHC wana project (mradi) yoyote ambayo
inaweza ikabadili hali ya miji yetu, tuwape nguvu wafanye hata kama ni
kidogokidogo, lazima tutoke kwenye hatua ya kuzungumza, kupanga na
kutembelea kujifunza, ni wakati wa kutenda,”alisema Zitto.
MWANANCHI
Post a Comment