Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima akitoa maagizo kwa wataalamu
kuwajibika kila mtu kwa eneo lake ili kuhakikisha anawaletea maendeleo
wananchi,Mkuu huyo wa Wilaya alitoa maagizo hayo wakati akifungua kikao
cha ushauri Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Septemba 30 2013.
(Picha na KIbada Kibada-Mpanda Katavi)
…………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi
Uharibifu
wa Mazingira katika wilaya ya Mpanda bado ni changamoto ambayo
inaashiria Wilaya ya Mpanda uoto wake kuharibika kila kukicha kutokana
na uharibifu unaofanyika wa uingizwaji wa mifugo kiholela,ukataji
miti,uchomaji moto mapori na uharibifu mwingine wa vyanzo vya maji
katika wilaya hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Selemani
Kakoso wakati wa kikao cha ushauri wa wilaya ya Mpanda kilichofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ulioko
Idara ya Maji Wilayani Mpanda.
Mbunge
huyo alieleza kuwa uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji katika
maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mpanda unachangiwa na uingizwaji wa
mifugo kutoka nje ya wilaya ya Mpanda wanaoingia kinyume na taratibu na
kwenda kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji.
Alieleza
kuwa zaidi ya asilimia 80 ya mifugo kutoka Mikoa ya Mara,Mwanza,Simiyu
na Shinyanga imekuwa ikiingia kwa kasi kubwa katika maeneo ya wilaya ya
Mpanda kupitia mkoa wa Kigoma na Tabora na kuchangia uharibifu mkubwa
wa maendeleo.
“Wapo
wafugaji wanaoishi kwenye vyanzo vya maji na hao ndio wanaochangia
uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali Wilayani Mpanda,alitupia
lawama Mamlaka husika hususani Idara ya Maliasili kwa kushindwa
kuthibiti uharibifu huo wa mazingira kutokana na kuwaacha wafugaji
wanaoishi kwenye vyanzo vyamaji viharibiwe na Mamlaka husika zikiwa
zinaangalia bila kuchukua hatua sitahiri.
Akizungumzia
Kijiji cha Bugwe ambacho kimetupiwa lawama na kutishiwa kufutwa au
kuhamishwa kwa kile kinachodaiwa kinachangia katika uharibifu wa
mazingira alieleza kuwa kijiji hicho wananchi wake hawahusiki na
uharibifu huo bali ni rafiki wa mazingira .
Alieleza
kuwa wanao husika na uharibifu huo ni wafugaji na wale wanaojihusisha
na shughuli za kilimo na makazi holela wapo watu ambao wanamakundi
makubwa ya ng’ombe walioko katikati ya Tarafa ya Mwese na Kabungu ambapo
ni eneo muhimu kwa kuwa ndipo vyanzo vya maji ya mito ipatayo
24,inayotegemewa na wakazi wa Mpanda na Hifadhi ya Taifa ya Wanyama Pori
ya Katavi na mito hiyo ndiyo inayotirirsha maji kuanzia kwenye vyanzo
vya maji,ambapo wanyama kama viboko wanahangaika kupata maji na wengine
kufa.
Alishauriwa
doria ifanyike kwa nguvu kubwa kuwaondoa wavamizi waliovamia katika
maeneo vya vyanzo vya maji na kueleza kuwa wengine wanakuja kununua
mifugo na kuipeleka katika maeneo ambayo hayaruhusiwi na wapo watu wengi
wenye mifugo mingi katika maeneo yanayolalamikiwa ya vyanzo vya maji.
Wapo
wajumbe walipendekeza kuwa wapige marufuku kwa mfugaji yeyote,kwa
wafugaji kuingiza mifugo katika wilaya ya Mpanda ili kunusuru mazingira
na uingizwaji wa mifugo katika wilaya ya Mpanda.
Kwa
upande wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Mpanda Patrick
Mwakyusa alikieleza kikao cha Ushauri Wilaya kuwa ni kukiuka katiba ya
nchi kumzuia mtu kuishi maeneo yeyote ndani ya jamhuri ya muungano kwa
kuwa nchi ni moja kosa ni kutofuata utaratibu wa matumizi bora ya ardhi.
Akafafanua
kuwa sheria ya ardhi ya kijiji imetoa mamlaka ya kupanga matumizi ya
ardhi hicho kijiji kinatakiwa kiweke mipango yake ya matumizi bora ya
Ardhi ili kuweka maeneo yanayohusika kwa matumizi husika.
Hivyo
ili kudhibiti uingizwaji holela wa mifugo katika vijiji ni kupanga
mipango ya matumizi ya ardhi hapo watasaidia kuondoa tatizo la
uingizwaji wa mifugo kiholela na kusaidia kuokoa vyanzo vya maji na
uharibifu wa mazingira.kwa kutenga maeneo ya matumizi bora ya ardhi
katika kijiji husika.
Awali
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alieleza alianza kwa
kuwasisitiza watumishi wafanye kazi kwa kujituma iwapo watawajibika kila
mmoja kwa nafasi yake wataweza kuepusha migogoro inayojitokeza katika
utendaji wa kazi kwa kuwa kila mmoja atakuwa anawajibika kwa nafasi
yake.
Hivyo
aliwasisitiza kila mtu kwa nafasi yae awajibike hapo ndipo matatizo
yatapungua au kumalizika kabisa katika maeneo mbalimbali,akizungumzia
kuondolewa kwa makazi holela alisema ipo operation inayoendelea
kuwaondoa wale wote wanaoishi katika maeno holela yasiyoruhusiwa kwa
kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu wanachangia katika uharibifu
wa mazingira.
Post a Comment