Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KISWAGA ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUINGIZA MAJI CHUMBA CHA MAITI HOSPITAL YA IPAMBA

 


Mganga  mkuu  wa Hospital hiyo ya Wilaya ya  Iringa  akimuonyesha bomba za maji zilizoingizwa katika  chumba hicho

Bw Kiswaga  akipokea maelekezo ya mradi  huo wa maji ambao ameutekeleza katika  chumba hicho  cha kuhifadhia maiti
Bw  Jackson Kiswaga akijaribu  kufungua koki ya maji kama ishara ya kuzindua rasmi huduma ya maji katika chumba  cha kuhifadhia maiti  Hospital ya wilaya ya  Iringa
Hapa  Bw Kiswaga akipongeza kwa  jitihada zake za klimaendeleo  jimbo la kalenga
Hiki ndicho chumba cha kuhifadhia maiti ambacho Kiswaga amejitolea  kuingiza maji
MKAZI  wa Nyamihuu jimbo la kalenga wilaya ya  Iringa  vijijini Bw Jackson Kiswaga ametekeleza ahadi yake ya  kusaidia  kuingiza  maji ya  bomba katika chumba  cha kuhifadhia maiti  cha Hospital teule ya wilaya ya  Iringa (Ipamba) baada ya  chumba  hicho kukosa bomba toka Hospital hiyo  ilipoanzishwa .

Kiswaga  ametekeleza ahadi  hiyo ukiwa ni muda  mwezi mmoja toka alipotembelea  Hospital  hiyo kwa lengo la kusaidia msaada  wa vitanda vya kujifungulia kwa  wanawake na kukutana na kero  hiyo ya chumba  hicho  cha kuhifadhi maiti  kukosa huduma ya maji ya  kuoshea maiti .

Akizungumza  baaada ya kutembelea  kuzindua rasmi maji hayo jana Kiswaga  alisema kuwa amelazimika  kutekeleza ahadi hiyo ya maji kutokana na maombi ya viongozi  wa Hospital  hiyo juu ya huduma hiyo ya maji.

Kwani  alisema hakujisikia  vizuri  kuona chumba hicho hakina huduma ya maji hivyo kujitolea kwake  kuweka maji ya bomba kutoaondoa adha kubwa ambayo ndugu  walikuwa wakiipata ya kuchota maji katika ndoo na kutumia  kuoshea maiti katika  chumba  hicho.

katika  hatua  nyingine  Kiswaga ameahidi kuboresha  zaidi eneo  hilo la chumba  cha kuhifadhia maiti  ikiwa ni pamoja na  kujenga banda maalum  la ngudu  kusubiri wakati  maiti ikiandaliwa .

Alisema  kuwa  akiwa akiwa kama mwana kalenga  ataendelea  kuwa karibu na Hospital  hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa  wana Kalenga na ndugu  zake  waliopo Kalenga hivyo iwapo ataiboresha  zaidi itakuwa ni mwanzo mzuri  wa  wananchi kupata huduma  bora  zaidi.

Kwa  upande  wake mmoja kati ya  wana kalenga  waliolazwa katika Hospital  hiyo Bw  Simon Sanga  alimpongeza Kiswaga  kwa jitihada zake na kuwa  wao toka miaka ya 1980  ambapo Hospital  hiyo ipo hawajapata  kuona kiongozi awaye  yeyote anayezungumzia kutatua  kero ya maji katika chumba  hicho cha kuhifadhi maiti na tayari viongozi mbali mbali ambao  walitangulia mbele ya haki  wamepata  kuhifadhiwa miili yao katika  chumba  hicho.

Mbali ya  kumpongeza Kiswaga  pia alisema kati  ya  wabunge  wote  waliopata  kuongoza  jimbo  hilo la kalenga hakuna mbunge  hata moja ambae  ameonyesha  kuliona  tatizo la maji ambalo Kiswaga amelitatua  na  kumtaka mbunge wa  jimbo  hilo Dr Wiliam Mgimwa badala ya  kuendelea kuwabeza  wanaojitolea  kuchangia maendeleo ya  jimbo la Kalenga  pia  kujaribu  kuisaidia  Hospital  hiyo ikiwa ni pamoja na kuwashukuru  wana kalenga wanaoishi nje ya jimbo  hilo ambao  wameendelea kujitolea  kusaidia maendeleo ya  wana Kalenga
 
MATUKIO DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top