NJOMBE, Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Njombe kuanza ziara ya wiki moja.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete atakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa mpya wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu kutangazwa Njombe kuwa mkoa ni pamoja kuzindua rasmi mkoa hu.
Katika
siku yake ya kwanza, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa
Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na
wananchi.
Katika
ziara hiyo ambako Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni
Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha,
Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa
Liganga.
Post a Comment