Mwanafunzi
wa darasa la nne shule ya msingi Bukokwa, Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza Cristina John (13) aliyeunguzwa na jiko la mkaa na dada yake
Paulina John baada ya kupoteza Mbuzi aliyekuwa malishoni.
Paulina
John aliyefanya unyama wa kumuunguza mdogo wake Cristina John bila
huruma na hajachukuliwa hatua zozote za kisheria huku vyombo vya dola
vipo na vinafanya kazi.(picha na Daniel Makaka, Sengerema).
Na. Daniel Makaka, Sengerema.
Mwanafunzi
mmoja aitwaye Cristina John mwenye umri wa miaka 13, ambaye anasoma
darasa la nne 4, katika shule ya msingi Bukokwa iliyopo kata ya
Nyakarilo wilayani Sengerema ameunguzwa jiko lilokuwa na mkaa wa moto
na dada yake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwn. Timoth
John wakati akiongea na redio Sengerema hivi karibuni amesema kuwa,
mtoto huyo ameunguzwa na jiko hilo lililokuwa na mkaa wa moto katika
makalio yake ikiwemo sehemu zingine za mwili wake, kwakile kilichoelezwa
kuwa alipoteza mbuzi wakati akiwa amewapeleka malishoni.
Amefahamika
kuwa tukio hilo limebainika baada ya mtoto huyo kuomba msaada wa
kupelekwa hospitalini kupatiwa matibabu, kutokana na maumivu
yaliyosababishwa na majeraha aliyoyapata.
Imeelezwa
kuwa baada ya kutoa taarifa kwa wananchi wasamalia wema walimchukua na
kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho, na kupatiwa matibabu na
baadaye taarifa hizo walizifikisha kwa Afisa mtendaji wa kijiji hicho,
huku wakilaani kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na mhusika anapaswa
kufikishwa katika vyombo vya dola.
Post a Comment