Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika harambee
ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa la Moravian Tanzania mjini
Sumbawanga akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aliyemteua kufanya hivyo baada ya yeye
kukabiliwa na majumu mengine ya kitaifa. Awali Waziri Mkuu aliafiki
mualiko wa Kanisa hilo katika kuongoza harambee hiyo ambayo imefanikiwa
kupata zaidi ya Tsh. Milioni 58 zikiwepo fedha taslim zaidi ya
shilingi Milioni 47 na nyingine zikiwa ni ahadi. Zimekuwepo pia ahadi
za mifuko 30 ya Cement na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani
hapo.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya akitoa neno la awali kabla ya zoezi hilo
la harambee kuanza ambapo aliwaomba waumini na wageni waliofika katika
hafla hiyo kutoa kwa moyo katika kuchangia kazi hiyo ya Mungu. Kwa
kuanzia alitoa ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa ambayo ni milioni tano
(5) na yeye mwenyewe kuchangia milioni moja. Aliendeleza harambee hiyo
kwa kuwachangisha kwanza viongozi wa Serikali alioambatana nao na
kuendelea na taratibu zingine kwa mujibu wa ratiba.
Askofu Mkuu
Conerad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa akitoa
neno katika hafla hiyo ambayo aliwataka waumini wa kanisa hilo kuchapa
kazi kwa nguvu na kuepukana na uvivu ambao alisema ni ugonjwa mkubwa
kuliko hata gonjwa la ukimwi. Alikemea pia tabia ya watu wengi
kuwahusisha watu waliofanikiwa kwa jitihada zao wenyewe na imani za
“Freemason” au “Ufisadi”.
Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika harambee hiyo
baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa mchango wake,
aliahidi mchango wa laki tano na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia
kanisani hapo.
Baadhi ya
viongozi wa Serikali waliohudhuria katika hafla hiyo, kulia ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela ambaye pia ni
mwanakamati wa ujenzi katika kanisa hilo, Katikati ni Mbunge wa Jimbo
la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Rukwa Mwaruanda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiendelea na zoezi la uchangishaji.
Baadhi ya
waumini wa kanisa la Moravian Sumbawanga wakimfagilia kwa shangwe
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal aliyachangia Tsh.
Milioni kumi zikiwepo za kwake binafsi Mil. 7 na nyingine Mil. 3
kuchangiwa na wabunge wenzake. Picha Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment