Mamlaka
ya hali ya hewa nchini- TMA imewatahadharisha wakazi wa jiji la Dar es
Salaam waishio mabondeni kuhama mapema ili kuondokana na adhari pamoja
na maafa yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazotarajiwa kunyesha
wiki ya pili ya mwezi Octoba na kutarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi
Desemba mwaka huu.
Akizungumza na ITV kwa niaba ya mkurugenzi wa
huduma za utabiri daktari hamza kabelwa meneja wa vituo vya hali ya hewa
Bw. Faustine Tillya amesema mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaamu ni
mwanzo mzuri wa mvua za vuli zinazotarajia kuanza wiki ya pili ya mwezi
Octoba ambapo ametoa wito kwa jamii nchini kujenga tabia ya kufuatilia
utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na mamalaka hiyo ili kuweza kuchukua
tahadhari.
Mhandisi mwandamizi wa kampuni ya mradi wa ujenzi
wa barabara ya mabasi yaendayo kasi -Strabag Bw. Hendrish Nyange
ameiambia ITV mvua zilizonyesha imekuwa changamoto kwao kujua mbinu za
kuhakikisha miundombinu ya maji taka ya barabara inaimarishwa huku
akitoa wito kwa wakazi wa jiji wenye tabia ya kuunganisha mabomba ya
maji machafu na kutupa taka kwenye mifereji ya barabara kwani inachangia
kuziba kwa mifereji hiyo na kusababisha maji kuingia kwenye makazi ya
watu.
Nao baadhi ya wafanya biashara wa Manzese Tip top
jijini Dar es Salaam wameilalamikia kampuni hiyo kwa kuondoa miundombinu
ya maji taka na kushindwa kuweka nyingine kwa wakati kitendo
kilichosababisha maji kujaa kwenye maduka yao na kusababisha baadhi ya
bidhaa kusombwa na maji .
Post a Comment