MAKAMU
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal amesema usimamizi wa haki za binadamu
na ujenzi wa maadili mema ndani ya jamii ni jukumu la kila mmoja hivyo
kila mmoja ana wajibu wa kulinda kuheshimu na kudumisha haki hizo.
Dk.
Bilal ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya Kimataifa ya Haki za Binadamu
na Siku ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Maadili katika viwanja vya
mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Alismea
Watanzania wakishikamana katika hilo, anaamini watashinda kwani umoja
ni nguvu katika kuhakikisha kuwa Haki za Binadamu zinalindwa na kupewa
nafasi stahiki.
“Nawaasa
kujiepusha na mambo yote yanayochangia kwa njia moja ama nyingine
kuvunja na kkukiuka misingi ya Haki za Binadamu na Maadili Mema, kuweni
raia wema na chukieni maovu” alisema Dk. Bilal.
Makamu
wa Rais aliwahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya awamu ya nne
inatilia maanani sana Haki za Binadamu Utawala Bora na Maadili.
Aliwaasa
Watanzania Tanzania kuanzisha kampeni Maalumu za kukuza maadili katika
ngazi mbambali zikiwemo za Utumishi wa Umma, Taaisisi za Dini, Elimu na
katika maisha ya kila siku.
Alisema
suala hilo likifanyika vizuri anaamini Watanzania wote watakuwa
wametimiza wajibu wao kwa malezi biora kwa watoto na vijana na kusaidia
kupunguza maovu mengi ndani ya jamii.
Alibainisha
kuwa Serikali pia imejenga mazingira mazuri na kuruhusu taasisi zisizo
za Kiserikali kuanzishwa kwa lengo la kusaidia juhudi zake za kuimarisha
Haki za Binadamu hapa nchini.
Alisema
hadi kufikia sasa Tanzania ina takribani mashirika 5,000 yasiyo ya
Kiserikali na yanayojihusisha na utetezi wa Haki za Binadamu, Mashirika
haya yanatambuliwa kwa mujibu wa mikataba mbali mbali ya kimataifa na
sharia za nchi.
Naye
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema kuwa Haki za
Binadamu ni kioo cha kuonyesha kuwa nchi yoyote ile imekomaa
kidemokrasia, hivyo inaheshimu raia wake kwa kuwapa haki zao za msingi
na katioka nchi zenye katiba zilizojengwa katika misingi kidemokrasia
kama ya kwetu
Alisema
serikali imeamua kuanzisha mpango kazi husika na kuratibu shuhuri hiyo
muhimu ya maadhimisho kwa kuhusisha tume mbali mbali za kitaifa.
Post a Comment