Wadhifa wa Urais wa Tanzania umeendelea kujikuta njia panda kila
unapofika wakati wa kuidhinisha kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa
waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na mahakama, na suala hilo limekuwa
gumu kutekelezwa katika awamu zote nne za uongozi.
Hukumu hiyo ni kama haitekelezeki na pengine
mafaili yaliyobeba uamuzi wa mahakama wenye adhabu za vifo, yameendelea
kusubiri kusainiwa tangu enzi za uongozi wa awamu ya kwanza wa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere na hata sasa Rais Jakaya Kikwete.
Watangulizi wengine wa Rais Kikwete ni Mzee Ali
Hassan Mwinyi aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Pili na Mzee Benjamin
Mkapa, aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Tatu. Wote wanatajwa kwamba
walikuwa wazito kuidhinisha utekelezaji wa hukumu hiyo ya kuondoa uhai
wa mtu.
Inaaminika kuwa Serikali za awamu ya kwanza na ya
pili zilitekeleza kwa sehemu hukumu hizo, lakini Serikali zilizofuata
hazikuwahi kufanya hivyo. Hii inamaanisha kuwa hakuna mtu aliyewahi
kunyongwa kwa miaka 18 iliyopita.
Takwimu zilizotolewa na Jeshi la Magereza kwa
gazeti hili zinaonyesha kuwa, hadi Oktoba 15, 2013 kulikuwa na watu 364
katika magereza mbalimbali nchini wanaosubiri kunyongwa, baada ya
kuhukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Taarifa hiyo iliyosainiwa na
Kamishna wa Magezera (CP), Dk Juma Malewa iliweka bayana kuwa hadi
wakati huo, wafungwa 86 walikuwa wamekata rufani za kupinga hukumu
katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema anasema hawezi kufahamu kwanini Marais wameshindwa kusaini hukumu
za vifo kwa muda mrefu, kwani suala hilo lina michakato na mambo mengi
ndani yake.
Hata hivyo anaongeza kuwa kutokana na Tanzania
kufuata utaratibu wa maadili (moral) katika utawala wake, inaweza kuwa
chanzo cha ugumu wa utekelezaji wake.
Hukumu ya Kifo hutolewa chini ya Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act. 1985) ambayo
inasisitiza kuwa utekelezaji wa hukumu hiyo ni muhukumiwa kunyongwa na
siyo vinginevyo.
Kifungu cha 322 cha sheria hiyo kinasema endapo mtu atahukumiwa kwa sheria hiyo, atalazimika kunyongwa mpaka kufa.
Utata wa kusaini
Akifafanua utaratibu wa kufikia hatua ya mwisho
katika utekelezaji wa hukumu hiyo, Jaji Werema anasema kabla ya rais
kusaini, hukumu hiyo hupitia Mahakama Kuu na ile ya Rufani.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment