|
Mheshimiwa Stephen Masele upande wa kushoto jukwaani akizungumza katika eneo la mkutano ambapo aliwaomba viongozi mbalimbali katika jimbo lake kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati,vyoo vya shule,masoko n.k.Hata hivyo alieleza kukerwa na baadhi ya madiwani katika jimbo lake hasa kutoka vyama vya upinzani wanaokwamisha miradi ya maendeleo mfano kata ya Masekelo,Ndala na Kitangiri. |
|
Awali
viongozi mbalimbali wa CCM muda mchache tu baada ya kuingia eneo la
Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo kata ya Kambarage mjini Shinyanga leo
jioni.Kulia ni mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri wa
madini Mheshimiwa Stephen Masele akiingia kwa kucheza wimbo wa CCM
uliokuwa unapigwa katika eneo la mkutano wa hadhara |
|
Mheshimiwa Stephen Masele ,akimkaribisha mheshimiwa Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoani Singida iliazungumze na wakazi wa Shinyanga |
|
Mbunge
wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba,ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa
CCM, akizungumza katika mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo
mengine aliwaomba wananchi wa Shinyanga kumuunga mkono mbunge wao
Stephen Masele kwani mbunge huyo kijana anayajua vyema matatizo ya watu
Shinyanga.Lakini pia aliwataka watanzania kuondokana na ugeni wa siasa
ya vyama vingi hivyo kupendana na kushirikiana na viongozi wao katika
kuleta maendeleo katika jamii hasa baada ya uchaguzi |
|
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia hotuba ya Mheshimiwa Nchemba katika eneo la mkutano |
|
Kushoto ni mheshimiwa Masele akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Nchemba |
|
Ndivyo
hali ilivyokuwa baadhi ya wananchi walikuwa mbali kidogo na eneo la
mkuatno lakini wanafuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo |
|
Mkutano unaendelea |
|
Mheshimiwa
Nchemba akimtambulisha kijana aliyejulikana kwa jina la Musa Tesha
mkazi wa Tabora(Kushoto) anayedaiwa kumwagiwa tindikali na vijana
wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA huko Tabora na
kusababisha kuharibika kwa sura yake.Akizungumza katika mkutano huo
kijana huyo amesema alitekwa na vijana wa CHADEMA,akapigwa,kuteswa na
kumwagiwa tindikali ,akapelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na
kuwashauri wananchi wa Shinyanga kukiepuka chama hicho. |
Wananchi wakisikiliza maelezo ya
kijana anayedaiwa kumwagiwa tindikali,ambapo kijana huyo alisema mmoja
wa wahusika wa tukio hilo yumo pia kijana mkazi wa Shinyanga
|
Mkutano unaendelea |
|
Mheshimiwa
Stephen Masele upande wa kushoto jukwaani akizungumza katika eneo la
mkutano ambapo aliwaomba viongozi mbalimbali katika jimbo lake kusimamia
kikamilifu miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati,vyoo vya
shule,masoko n.k.Hata hivyo alieleza kukerwa na baadhi ya madiwani
katika jimbo lake hasa kutoka vyama vya upinzani wanaokwamisha miradi ya
maendeleo mfano kata ya Masekelo,Ndala na Kitangiri. |
|
Mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo wakiwa eneo la mkutano
credit: Kijukuu blog |
on Monday, December 30, 2013
Post a Comment