Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha bunduki aina ya Shotgun waliyokutwa nao watu hao.
Afisa wa polisi katika ofisi ya kamanda wa polisi akipanga vitu mbalimbali walivyokutwa navyo watu hao wanaotuhimiwa kuwa majambazi.
Laptop mbili pia zilikuwa ni miongoni mwa vitu walivyokutwa navyo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha Vocha za mitandao mbalimbali walizokutwa nazo watu hao.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi
JESHI la polisi mkoani Kilimanaro, limewatia mbaroni watu 4 kwa
tuhuma za kushiriki katika matukio mbali mbali ya uhalifu na
unyangaji wakutumia silaha yaliyotokea mkoani hapa.
Kaimu kamanda wa jeshi hilo, Koka Moita, alisema jeshi hilo
lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao baada ya kukamata gari
lenye namba za usajili T564 AUW aina ya Grand Mark 2 wenye rangi ya
siliva, katika maeneo ya Kiusa Manispaa ya Moshi ambalo limesadikika
kushiriki kwenye matukio hayo.
Alisema dereva wa gari hilo ambaye alifahamika kwa jina la Nicksoni
Elias Urio (28) mkaazi wa Majengo Moshi alitoa ushirikiano mkubwa
ambao ulipelekea kuwakamata watu 3 ambao wamesadikika kuwa majambazi
walioshiriki katika baadhi ya mtukio mkoani hapa.
“ Baada ya kuwatia mbaroni watumiwa hao, operatini kali ilifanyika
yakuwapekuwa na kubaini vitu mbali mbali ikiwemo ikiwemo bumbuki
aina ya shotgun ikiwa imekatwa mtutu na kitako cha bunduki hiyo hivyo
hatukupata namba zake”alisema na kuendelea kuwa
“laptop, 2 aina ya dell na hp, Plate namba 3 na funguo za magari,
simu 8 za mkononi , vocha za simu za mitandao yote , ambaye thamani
yake haijatulikana, pamoja na vifaa mbali mbali vya kuvunjia”alisema
Moita.
Moita alisema Vocha za simu bado hazijajulikana thamani yake, na uchunguzi unaendelea marautakapokamilisha watuhumiwa watafikshwamahakamani.
Moita alisema Vocha za simu bado hazijajulikana thamani yake, na uchunguzi unaendelea marautakapokamilisha watuhumiwa watafikshwamahakamani.
Aidha Kamanda Moita aliwataka wananch kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi
la polisi ili kufichua matukio mbali mbali ya uhalifu yanayojitokeza
mkoani hapa.
Post a Comment