HATIMA
ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Zitto Kabwe na wenzake wawili, itajulikana Januari 3,
mwakani, watakapoitwa mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho kujitetea.
Mbali ya Zitto, viongozi wengine waliovuliwa madaraka Novemba 22, mwaka
huu, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba
na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo.
Zitto na wenzake walivuliwa madaraka baada ya kubainika kuandaa waraka wa siri wenye lengo la kukigawa chama hicho.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari Mwandamizi wa chama hicho, Tumaini Makene, alisema Zitto na wenzake wanatakiwa kufika mbele ya Kamati Kuu baada ya kuandikiwa barua ya wito na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa.
“Ni kweli Zitto na wenzake wanatakiwa kufika mbele ya Kamati Kuu Januari 3, 2014, saa 2 asubuhi, hii ni kutokana na barua ya Desemba 28, mwaka huu, waliyoandikiwa na Katibu Mkuu.
“Katika barua hii wametakiwa wafike bila kukosa ili wajieleze kwa mdomo, baada ya kujibu tuhuma 11 zilizokuwa zikiwakabili baada ya kuvuliwa nyadhifa zao hivi karibuni.
“Ukisoma vizuri Katiba ya CHADEMA, kifungu cha 6 (5.2)b na 6 (5.2) d, kinasema Kamati Kuu inaweza kuitisha kikao cha dharura, hivyo nasi tumezingatia hili,” alisema Makene.
Alisema baada ya viongozi hao kujieleza kwa barua zao, waliwasilisha utetezi wao na Desemba 18, mwaka huu chama kiliwaandikia barua ya kuwajulisha utetezi wao kuwa umepokelewa.
Alisema kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Miongoni mwa mashitaka ya Zitto, Dk. Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya chama inayokataza kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa hilo, wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe, Katibu Mkuu Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.
Moja ya madai katika mashtaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote.
Zitto na wenzake, wanadaiwa katika kosa la pili, kutokuwa wawazi na wakweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha 10.1 (VIII).
Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).
Katika kosa la nne, wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama, miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Kosa la tano, wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Katika kosa la sita, ambalo mtoa habari wetu alisema ndilo kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwa kutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.
Hatua hiyo, inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa 2012.
Zitto na wenzake katika kosa la saba, wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa Kuwania Uongozi. Katika kosa la nane, Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.
Katika kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na kosa la kwanza, ambalo washitakiwa wanadaiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na Lema.
MTANZANIA

Post a Comment